Arteta amenisikitisha sana kumsajili Kai Havertz. Hii inaonesha kwamba mpaka sasa hajafahamu mahali tatizo la Arsenal lilipo.
Paundi 65m kama angetulia na akaziongezea kwa kumuuza Balogun, Tavares na Nketiah angeweza kumleta pale Osimhen. Kai sijui amemleta kufanya nini.
Usajili wa Declan Rice na Timber ni mzuri na kwa sehemu utasaidia kuimarisha kiungo na ulinzi lakini still Arsenal inahitaji goalkeeper ambaye yupo serious.
Wachezaji wa kawaida kama Reiss Nelson, Fabio Vieira, Rob Holding, Cedric Soares, Nicolas Pepe na Sambi Lokonga wanatakiwa kuondolewa haraka.
Msimu ujao nategemea Arsenal itabakia kwenye top four lakini masuala ya ubingwa tuendelee kuyasahau.