Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Daaah hamis77 unajua kuchambua soka au unavyanzo makini Sana vinavyoelezea soka

Nabii hakubali kwako, ila kiukwel jf nzima hakuna anaeweza ku-match na wewe. Mz uyee upo vizuri Sana sanq Vu I got

I wish siku moja uwe redioni au kwa TV live.
Sasa hapo kachambua au ka-copy and pasteana uwezo wa kuandika lugha hivyo?acha kumpa sifa za kijinga Aunt Hamis
 
City mara nyingi amekuwa ananufaika anatukuta hatuna key players wetu wengi

Uliona Community shield alitukuta Jesus hayupo ,wengi walikuwepo ,uliona mziki wake

Sasa leo tutaishi nae vzr atake asitake


Kuna mechi tulimkamataga Sana hapo Emirates,Refa akaingilia Kati kuwasaidia tukanyimwa penalty wakaja kupewa wao na tukapewa Red
Hii game naikumbuka
Before red card, ngoma ilikua 50/50 octopus partey anachafua tu dimba

Yule Refa mpuuzi akaanza kumtoa umeme partey
 
Hakuna anaye mfananisha na xhaka, ila jamaa uwezo bado mdogo sana Hakuna alicho ongeza kwenye Team.
-Angalia sajili ya Rice na ina impact gani kwenye Team.
-Same kwa Timber kabla ya injury unaona kabisa kuna kitu tuna benefit uhitaji kutumia akili nyingi.
-Sasa uyu KAI Mnajikuta mnachambua Details za kijinga ambazo hazina mchango wowote kwenye Team.
niliangalia mechi ya Monaco jana na Balogun akaifunga Reims Timu yake za zamani na hakushangilia goli,ilikuwa ni upuuzi kumruhusu a young talented kama Balogun kuondoka na kubaki na MAGARASA kama Nketiah na hili kubwa jinga Kai Harvetz,tena huyu Kai ndio hakuna chochote alichoongeza kwenye Timu licha ya kununuliwa kwa Pesa nyingi,huwa nashangaa humu JF wanavyomsifia kwa ku-win sijui mipira ya juu,sijui kuimpresshakika nashindwaga kuelewa,leo akianza lazima tugongwe mapema sana
 
Arsenal fans huwa hatumpi heshima yake Martinelli ,nadhani mechi mbili tatu hizi tumemisi Sana shughuli yake


ESPN walitaja mawinga 100 Bora duniani , Martinelli yupo 10 Bora


Pia Ni mchezaji wa 7 EPL na 23 duniani kwa kuwa na Thamani kubwa .


But tumekuwa tuna mu underrate na kumchukulia kawaida

Speed
Goal scoring
Track back
Energy
Dribbling

Nadhani Sasa tutaanza kumpa heshima Kama tunayompa Bukayo saka
Huyu jamaa nilikuwa namchukulia poa sana. Ila sasa hivi ndo nimeuona umuhimu wake.
 
Kwamba picha za mazoezi zimefichwa

Ila utoto raha sana kama kombolela vile.
Kuna kauli wanatoa mashabiki wa Manchester united, unaona huu ni utani tuu na mbwembwe za mashabiki. Mfano zile kauli za "Leo ndo tunaanza ligi" wakati ni matchweek 10+.

Ila hawa jamaa humu, mambo wanayosema sio kwa utani, bali ni wanaamini kabisa kama yanawezekana. Mfano Cha-mbuzi Hamisi anadai timu tishio UCL ni Man City tuu. Hii sio kauli tuu, bali ndo imani anayoiamini plus chawa zake.

Wanaamini UCL wao wanaanza round of 16, katika makundi wanamaliza na points 15 mpaka 18.

Na hilo ndo linalifanya hili jukwaa lionekane ni la vichekesho. Ndo maana wengine majukwaa mengine hukuti timu pinzani zikishinda mule. Ila humu, everyone anaona ni jukwaa la utani la Arsenal
 
Kwamba picha za mazoezi zimefichwa

Ila utoto raha sana kama kombolela vile.
Mbona kawaida hiyo Kaka ,umeanza kuangalia Mpira lini


Mech Arsenal vs Manjesta tuliyowapiga 3-1

Siku moja kabla Partey aliumia ,ikafichwa ili tusiwasanue ,japo kuna mwana alivujisha ,Arsenal wakatoa picha Partey yupo mazoezin ,lakin ukweli siku hiyo hakufanya mazoezi

Na kwenye mechi hakuwepo ndio karud juzi tu
 
Gabriel Martinelli ameharakisha kupona kwake kutokana na jeraha la msuli wa paja ndani ya saa 48 zilizopita.
Swali ni je atajumuishwa kwenye kikosi.

Saka alifanya mazoezi siku ya Jana na leo Jumapili.

@SamiMokbel81_DM
 
Tusijipe matumaini sana, mechi ya leo ni ngumu, lolote linawezekana; ndio maana hata odds hazitofautiani sana
Mpira una matokeo matatu

But hii haizuii Mashabiki kuwa na Iman na timu Yao

Hata wao Mancity wanaogopa pitia platform zao

EPL Hakuna mchekeamchekea ,

Wanakuja kwetu lazima wawe na adabu
 
Kwamba picha za mazoezi zimefichwa

Ila utoto raha sana kama kombolela vile.
Nimeshangaa Sana kutojua hivi vitu, hujawahi kuona mchezaji hakuonekana mazoezin kaja kuonekana kwenye mechi

Juzi hapa tulikuwa na injury Kama 5 na hawakuoneshwa kwenye picha za mazoezi ,

Mechi na bornamouth wakawepo ,Mpira Ni mind game sio kwenda kichwa kichwa Kama 7HAG had Sasa ana majeruhi 10

Arsenal hawakutoa picha za Saka za mazoezi sababu timu ya Taifa nao wanamtaka ,baadae wakatoa majina wamemuita baada ya kupewa taarifa yupo fit

Mwisho Arsenal watakaa na FA baada ya Leo kuomba Saka asitumike NATIONAL TEAM ili apumzike
 
John stones, Bernado silva & Rodri (red card) .
Ni mara nyingi tu Arsenal wamewakosa wachezaji muhimu dhidi ya City i.e Partey, Saliba etc, hiyo ni hali ya kawaida mchezoni, ni kama vile Arsenal watavyomkosa Timber au Gabriel Martinelli, au maybe Saka. Mwisho wa siku mpira lazima uchezwe, No excuses.
 
Hao Ni watu wenye akili ndogo ,thus why nimepunguza kujibizana na wengi sababu akili zao Ni ndogo

Akili kubwa kujadiliana na akili ndogo ni upotevu wa muda na pesa maana natumia MB


Mimi nataka mtu ani challenge kweli kweli sio bla blaa

Mtu hajui mchezaji anacheza eneo fulani Sababu ya roles yake ,

Mtu hajui kuwa klabu ina mitambo ya kukusanya data zakila mchezaji kwa kila parameters ambazo ndio huamua acheze mechi .


Wengi humu Wana knowledge ndogo Sana ya mpira wameingia kwenye ushabiki sababu ya kubeti


Akiliwa pesa ya mboga anaamini Kai ndio kamkosesha
We jamaa bhn
 
Mimi kusema kule UCL timu ngumu Ni city ukitoa wengine ungaunga anachukia


Yalianza makampuni ya ubashiri yaliweka kwa ascending Order

Mancity
Baryen
Madrid
Arsenal

Nikasema Madrid hatishi Tena hata magoli kwasasa yanafungwa Sana na Jude , je Jude atafunga kila siku ?

Nikasema Madrid pia hawana a world class GK na CF

Bayern pia Ni unga unga ,Hana beki nzuri anaruhusu Sana magoli ,Hana a no.6/DM wakueleweka

Tuliona Bayern alivyocheza na Manjesta iliyojichokea ,walioangalia Bayern na Copenhagen watakuwa wanaelewa jinsi Bayern alivyokuwa anasumbuliwa

But kwa factors hizi Ni dhahiri hao Wawili hawana Quality kama ya mancity wamewekwa juu ya Arsenal kwa kigezo kimoja tu Ni wazoefu na big teams .


So Mimi kumuona mancity ndiye mgumu pekee UCL mtu anaumia .

Huo ndio ukweli


Tukutane may Pale Wembley Fainal
 
Back
Top Bottom