Arsenal (The Gunners) | Special Thread


Ungeweka na wewe ushabiki pembeniii, Ramsdale kacheza game zaidi 36 epl last season na kaziweza sana tu. Kacheza na Brighton, brentford na timu nyingine nyingi tu za pressing na alikua poa tu, yaani unaongelea kipa aliyecheza match zaidi ya 36 epl kushindwa game ya Lens?.

Ramsdale amemtoa leno kwenye choice no 1 kutokana na ability yake hiyo hiyo ya footwork

Ramsdale ameshafanya save nyingi sana za maana kushinda hata huyo Raya, unavyomsema ramsdale hapa kuwa game ingemshinda ni kama vile unamuona ramsdale ni kipa choice no 3 vile or ni kipa ambaye sio mzoefu yaani ramsdale game vs Lens ndo ingemshinda
game na city , Liverpool, brighton zote kaziweza ndo hii imshinde kweliii
.
 
Ongea yte mkuu uwanja ni wako🤠🤠🤠....yamebaki masaa kadhaa tutakutafuta uje utuelezee imekuwajekuwaje matokeo ya mechi yenu...tupo hapa🤠🤠🤠
 
Ongea yte mkuu uwanja ni wako
....yamebaki masaa kadhaa tutakutafuta uje utuelezee imekuwajekuwaje matokeo ya mechi yenu...tupo hapa

Hapo nimeweka ushabiki pembeni mkuu, kuona ramsdale hafai eti game ya lens ingemshinda huo ni uongo na unafiki wa hali ya juu sana. Ramsdale huyu huyu kawaokoa match against big teams zenye striker wa maana then anatokea mtu anasema game na lens ingemshinda haya si maajabu yani unamuongelea ramsdale kama vile unamuongelea hein au turner .

Wewe tulia ushapigwa misumari 2 na lens , uone kesho kikosi cha maana kinacheza PSG kaingia kwa mtakatifu james pale chochote kinaweza kutokea . Halafu group letu unalijua ni group la namna gani so ni timing PSG akiingia kwenye mfumo usishangae kuona anakufa kamba za kutosha.
Hili ni group la kuwaiana atakayewahi ndo huyo huyo mshindi


Njoo uone maana ya kikosi kipana sio nyie kila game wachezaji walewale tu Newcastle tunapiga rotation ya kutosha kama vile rotation formula zile I=∑mir2i.
 
Tukiacha makosa binafsi ya wachezaji ambapo ni kawaida kwenye mpira, lakini tatizo la Arsenal linaanzia na Kai Havertz... Tutaonekana tuna chuki lakini ukweli ni kwamba tujiulize huyu mchezaji ameipa Arsenal kitu gani kipya ambacho Arsenal msimu uliopita walikikosa? Zaidi ni kuifanya Arsenal kuwa very Shamble kule mbele lakini bado anapewa gametime ya kutosha kuliko uwezo wake wakati nje tuna watu ambao wana uwezo wa kufanya attacking kuliko Havertz. Shame on Mikel Arteta. Mashabiki wa Arsenal wengi ni wanafki sana na hawajitambui wanataka nini. Nilishangaa sana hata mechi iliyopita anaimbiwa nyimbo kisa kafunga Penalty. ESR kwa uwezo wake sioni sababu ya kuendelea kubaki Arsenal, kuna muda mapenzi na timu inabidi uweke pembeni uangalie future zaidi. Amefika kwenye umri ambao inahitaji kucheza sana kufika kwenye peak yake. Sio kukaa nje na kumuangalia mtu mvivu na jinga moja kama Kai Havertz linaanza juu yako. Huko ni kudharauliwa.
 
hamis77 utatukanwa sana.. Ni vile watu wengine hapa tunaheshimu mawazo ya mtu na hatuna kauli kali. Ni ngumu mtu kumuaminisha uongo kwa watu wenye uelewa na hicho kitu. Inatia hasira sana aisee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…