Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Mikel Arteta:

"Emotionally, winning is the best, the best, the best.

It is the best thing you can do, and I now have 24 players desperate to play on Sunday." [Arsenal]
 
Good game kwa Kai leo.

Ila acha niungane na akina Hamisi (masingeli by flano), kuhusu kumpa muda Kai na kuzidi kumpa sapoti.

Some of Arsenal fans ni kama tunataka afeli jamaa. Huku banda umiza, Kai akiwa na mpira tuu, basi mashabiki zaidi ya 10 unawasikia wakisema "anapoteza sasa hivi".Mara amefanya hivi, angefanya vile.

Nadhani tunachokitaka fans kutoka kwa Kai, na anachokitaka Arteta ni tofauti kabisa kama alivyowahi kugususia mkorea (chawa wa masingeli by flano) Its better tukaendelea kumuamini Arteta.
Tulimsubiri Pepe kwa misimu yote 4 kwamba ipo siku ataonyesha uwezo wake.

Kai huko alipotokea hakua na impact yoyote na wao walisubiri misimu 4 afanye la maana ila wapi. Cha ajabu sisi tunampa huo muda kwenye mechi muhimu, kwanini asianzie benchi ajifunze taratibu? Atakuja kutucost kwenye mechi ya muhimu kisa hizi experiments.
 
ZittoJr ,kuna kipindi ulisema Rice bado hajai. Master ile DM inamshinda na mimi nilikubaliana na wewe, ila kwa nilichokiona toka game na Wale Seleman (Nyumbu) had game ya leo PSV nimekubalo kua Rice ni Dm Pure kabisa na kaiweza kui master vzr kwa aslimia zote

Vipi kwa upande wako Rice bado haiwezi ile DM?
Ilikua wazi kabisa kuwa Partey alikua better kipindi kile ndio maana kocha aliwaweka wote wawili Kila mechi Ili ajifunze taratibu but Rice alikua na ubora tokea akiwa West Ham ilikua ni suala la muda tu.

But Kai tokea Chelsea ni mzigo alafu ni mzito sijui mvivu Kuna goli la wazi kabisa kakosa Jana alafu Kuna counter Moja tulipiga badala atoe pasi nzito akapiga kama hataki counter ikafa.....

Yule sijui analeta Nini mezani, maybe naye apewe muda ingawa kama hakuonyesha huo ubora Chelsea basi tutasubiri miaka 3 mpaka tukiri ilikua hasara.
 
Mtazamo wangu:
Raya Yako vizuri. Sijaona kama amemzidi Ramsdale sana na ni premature kumpaisha kuliko Ramsdale kiasi Cha kumfanya Ramsdale aonekane mbovu. Siyo poa. Nilisema positioning yake katika build-up inaacha goli exposed sana. Nimependa kwamba anaonekana anaweza kudistribute vizuri tu na miguu yote miwili, ila sijaona kama ana utulivu sana akiwa pressed.

Rice hayuko vibaya, ila sijaona kama anamzidi au hata kumkaribia Partey katika DM. Bora wacheze wote kama Partey yupo, na Mimi ningemuweka nafasi ya Kai, acheze double 8 na Ode.

Kai namchukulia kama Xhaka. Yaani apewe muda zaidi wa kufanya kazi na Arteta na Arsenal. Ila Kai ana kazi ya kupambana kisaikolojia kwanza maana Yuko under pressure sana na inaonekana watu wanaomuangalia wengi wanaona na kutafuta kuona makosa yake zaidi ya mema yake. Hapa ni tofauti na Raya ambae watu wanatafuta mema yake tu na mapungufu hawayaoni au wanayapuuzia.

Kama Arteta aliweza kumgeuza Xhaka kutoka kukaribia kuondoka hadi kuwa key player, naamini anaweza kufanya hivyo Kwa Kai Kwa position hiyo pia. Ni Kai mwenyewe pia kubalika na kuongeza attitude ya kuwa sisi tunataka kuattack na aache kuua moves Kwa kurudisha mipira nyuma. Jana tena kapewa bonge la pass na Raya ila akashindwa kugeuka na kupelekea mpira mbele, badala yake akarudi nao tena nyuma na move ikafa. Kwa mambo haya, wenzake wataanza kumbagua kwanye pasi, wakipendelea kubuild up wenyewe labda hadi wafike mbele, wapige cross, Kai apige kichwa ndiyo involvement yake iishie hapo.

Saliba naye ni mnyama hatari. Naanza kuona na kuamini zaidi kuwa injury yake last season imechangia zaidi ya 60% kutupotezea ubingwa last season. Nadhani jana nimeona zaidi ya mara moja akiwa under pressure kutoka Kwa forwards wawili akiwa anamface kipa lakini badala ya kupiga back pass, akawageuza mithili ya Jesus na kuanzisha attack. Saliba anakufanya uhisi kama Kuna Odegaard mwingine kule nyuma na attack nyingi nzuri za kibunifu zinatokea kwake. Huyu jamaa atafutiwe namna ya kupumzishwa asichoshwe au kuumizwa. Gabriel naye atafutiwe njia ya kulindwa. Yeye na Saliba ni combination Kali sana kwetu.
 
So far wanataka mchezaji afeli ,hii Tabia wameitoa kwa mashabiki wa nyumbu

Ila ukishajua Kai anatumikaje Arsenal Wala hutaingia kwenye hiyo mitego

Kai am, Trossard,rice,Vieira wanacheza LCM but kila mmoja ana majukumu tofauti na mwenzake

Mfano Kai majukumu yake acheze LCM lakin awe Kama second CF,


Jana kaanza mechi Kama LCM kamaliza Kama false 9

So Kai ataendelea kucheza sababu anatimiza majukumu yake vzr tu

| Mikel Arteta on Kai Havertz playing different roles in the game:

“He was very connected today in the game. It’s true that I ask him to play in two different roles in regard to the opponent’s behaviours. He’s so intelligent the way he does it. It’s just finishing one or two actions that we had again, but it’s coming and he’s so willing to do it.”

[@arsenal]
Kai apewe muda.
 
Fabrizio Romano says Brentford want 'something around 50 or 60 million pounds' for Ivan Toney.

Chelsea and Arsenal are 'well informed'.
 
USARA ZA GWIJI WA HIGHBURY UCL RETURNS

Nianze kusema pengine Wengine watafikiri PSV ni wabovu hapana bali Arsenal ndio kawafanya waonekane inferior

Kufika Game Dhidi Arsenal walikuwa hawajapoteza Mchezo wowote kwenye michezo yao 25 iliyopita ( Unbeaten run )

Nakifikiri unaweza kupata picha kwamba Arsenal alikuwa superior kimbinu kimchezo kumzidi PSV

Nianze kusema Kitu cha kwanza ambacho kiliwashitua Wengi Ramsdale kukaa bench Match 2 mfululizo ila kadri match inaendelea tactically nilielewa kwanini

Arteta Anahitaji kutawala mchezo ili utawale mchezo lazima mpira ukae mguuni kama nikuanza pass Nyuma au kupiga mipira mirefu kuwepo na Accuracy

Raya distribution yupo vizuri sana ni mtulivu na pass zake nyingi uhakika game Everton baada Arsenal kuongoza goal 1 raya alipiga pass sahihi 11 kati 12 kitu kinafanya arsenal kuendelea kutawala mchezo

Match PSV long balls Raya kapiga pass 12 sahihi kati 17 alizojaribu hii ni zaidi nusu ya pass zake zote ndefu ziliwafikia walengwa

Sisemi Ramsdale Hawezi ila siku karibuni ata mwishoni msimu jana accuracy ya pass Ramsdale imepungua per 90minutes

Game palace baada sisi kuongoza alikuwa anapiga mipira mingi mbele inapotea hivyo pressure inarudi langoni kwetu au tunapoteza control mpira

Nafikiri Arteta anafanya hivi kumpush Ramsdale arudi kwenye best version yake yule aliyetoka Shelfield

Yote kwa yote tumecheza vyema kucontrol mchezo kucreate nafasi na kutumia madhaifu defense ya PSV kwenye marking kuwamaliza

kilichopoteza zaidi ni positional interchange ya Saka, Trossard , Ode , Kai hivyo kusabisha kuacha baadhi wachezaji Isolated na wakawaadhibu goal la trossard na Odegaard walikuwa isolated bila Marking adi wanapiga

North london derby here we come

Amigos
 
Kuna siku Raya atakuja kutoa assist akiwa golini.

Jamaa ana footwork bora kabisa, maybe the best in PL..

Na distribution ndio si mchezo.

Kuna siku itapigwa counter attack kutoka kwa Raya mpaka kwa Saka/Martinelli, nitakuja kuifufua hii post!

David Raya Martin.. Remember the name.
Snapinsta.app_379313811_325679069924664_336700192376670416_n_1080.jpg
 
Nilisema baryen na Madrid sio tishio Tena

Flano na Genge lake mkohoti wanakwambia Ni uzushi

| Bayern Munich so far this season:

6 games
4 wins
1 draw
1 loss
️ 14 goals scored
10 goals conceded
️ 1 clean sheet
Yaani Masingeli unatoka kucheza na PSV halafu anakuja kuwakandia Bayern na Madrid kua sio tishio?
Haya maneno unatakiwa uyaongee ukiwa umeshacheza nao na kuwafunga.
Kama unaona ni rahisi kumfunga Bayern goli 3 kama Man Utd tulivyofanya basi muulize mzee Wenger nini kilimpata alivyokua anataka kupishana na Wajeremani.
 
Jana nimemuangalia, alicheza vizuri
Cha ajabu wanaomuangalia makosa tu wanakwambia hajafanya kitu

| Tim Sherwood: “Kai Havertz, for me, he’s not started the season but he looks a real player tonight,”

“He’s got so much room to operate in. He’s not shy of a Champions League goal in the final, is he?”(sky via tbr)
 
Yaani Masingeli unatoka kucheza na PSV halafu anakuja kuwakandia Bayern na Madrid kua sio tishio?
Haya maneno unatakiwa uyaongee ukiwa umeshacheza nao na kuwafunga.
Kama unaona ni rahisi kumfunga Bayern goli 3 kama Man Utd tulivyofanya basi muulize mzee Wenger nini kilimpata alivyokua anataka kupishana na Wajeremani.
Baryen unayoizungumzia sio hii, na Arsenal unayoizungumzia sio hii elewa Hilo

Baryen na Madrid Ni wakawaida huo Ni msimamo wangu toka hata makund UCL hayajapangwa ,

PSV ana unbeaten run ya 20+ mechi, kwenye Ligi ya uholanzi ambayo 7hag mnadai alifanya vzr na mnamuita kocha Bora ,PSV hajafungwa had Sasa

Madrid kacheza na kibonde kuliko PSV ,kapata goli dakika 94

Sasa usimdharau PSV , Arsenal kwasasa tunatoa mbinyo wa maana
 
Jana nimemuangalia, alicheza vizuri
Kai ataendelea kucheza sababu anatimiza aliyotumwa

️ | Another decent performance from Kai Havertz. He is just lacking confidence in front of goal. The rest of his output is fine.

90 minutes played.
46 touches.
93% pass accuracy (25 completed).
1 key pass.
1 big chance created.
6 ground duels won.
3 aerial duels won.
7.0 rating (@SofascoreINT)
 
Nasikia Arsenal wameshaamza mazungumzo nae chini kwa chini huenda akajiunga January

Mikel juz kasema anataka kila namba iwe na watu wawili wenye uwezo sawa

Eddie bado hampi changamoto Jesus
Tukimpata huyu jamaa tutakuwa na luxury ya kutosha pale mbele....maana kuna mechi unaweza ukaanza na Jesus kama right wing na toney pale kati....Saka akapumzika maana anacheza mechi nyng sana kwa sasa....si nzuri kimwili
 
Back
Top Bottom