Wakati Xhaka anacheza ilikua timu ikipata mpira anaenda kuhold kushoto kwenye mid ili kutoa support kwa Martinelli au kumpa chance Martinelli ya kuoverlap.
Kisha timu ikiadvance anakua nje ya box. Kutegemea na attack anaweza na yeye akaingia kwenye box au akaendelea kubaki hapo. Kwakua Xhaka hana mbio nahisi hakua anarisk kujisahau kuingia kwenye boksi kwakua angeshindwa kurecover.
Pia Xhaka alikua anatoa pass kushoto, kulia, mbele na nyuma.
Kai timu ikipata mpira instinctively unamuona anazama deep kwenye next phase ya attack kwamba sasa ushamuona anaenda mpelekee mpira au ucheze naye 1 2.
Ila Kai hana vision. Siyo mzuri kwenye accuracy ya pasi lakini pia kwa timu yetu na jinsi yeye anavyoanza kukimbia namna pekee anaweza zicheza 1 2 ni ama iwe counter au amuone Odegaard upande wa kulia anavyoushughulikia. Ile instinctively kukimbia mbele wenzake wanashindwa kumpa mipira kisha mtazamaji naona anafanya iwe ngumu kugewa mpira muda goli linatafutwa na kuona jamaa anakimbia pasi.
Timu imepiga jumla ya pasi 520 katika hizo Kai ni amegusa mpira mara 45 tu na imemfanya awe wa mwisho. Pia ndiye aliyepoteza mpira mara nyingi.
Kuna mshkaji kamuuliza
zitto junior kwamba kwa Rice ulisema hivi na vitu kama hivyo.
Yaani shabiki anaona uvivu kucounter hoja hivyo anaamua kukuletea ukumbusho kumaanisha kwamba ulishawahi kukosea once so hata hapa hauwezi kua sahihi. Zitto naye akianza kufukua vitu kuonyesha kwamba alishawahi kua sahihi hata mara 100 hua mnakasirika.
Timber kacheza mechi moja na wote tukasema hapa tuna mtu.
Rice ananunuliwa kabla ligi haijaanza nikasema kumuuza Partey kisa Rice kaja ni risk, wabaki wote kwanza kipindi Rice anazoea mazingira. Well game ambazo Partey alikuepo tukakubaliana humu kua kweli Partey ilibidi awepo ili Rice azoee polepole.
Wakati tunasema hivyo Rice hakua mbaya, ila hakua anafanya alichokifanya kuanzia game ya nne (hesabu kuanzia ya City) ile siku jamaa alionyesha upande mwingine kabisa mpya na ndiyo yupo nao mpaka mechi ya mwisho mimi kuona.
Rice ameadapt fasta. Timber kaja na kuonyesha haimsumbui kukaa kule kulia. Kai bado anajitafuta, ndiyo kusema hatutakiwi kusema kua jamaa anajitafuta? Hata sisi tusiposema takwimu zinasema. Kila game zitaonyesha mchezaji kafanya nini, akifanya sawa watu wakibisha takwimu zitasema pia.