Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

last time i checked walitufunga kwao .. tukaja wachinja emarates.. mara nyingi inakuwa hivo ...
Hapana mkuu! usitazame ya msimu mmoja tu uliyopita.....jaribu kutizama misimu kama saba mfululizo bila kusahau na FA.
Hata kwenye mtanange huu wa leo utaona Arsenal watacheza vizuri kama Barca,lakini mwisho wa dk 90 utaona Man u 3 Arsenal 0 au 1.
Sasa hapo ndiyo huwa nashindwa kuelewa! tatizo ni nini?
 
Leo hao lazima wanywe nyingi sanaaaaaaaaaaaaa,maana na kikosi chao kibovu sijui itakuwaje........
 
last time i checked walitufunga kwao .. tukaja wachinja emarates.. mara nyingi inakuwa hivo ...

Mkuu hiyo ya last year ila kwa mwaka huu kazi nzito kidogo mnayo coz hamna squad nzuri na ya kufurahisha
 
Leo hao lazima wanywe nyingi sanaaaaaaaaaaaaa,maana na kikosi chao kibovu sijui itakuwaje........
Mkuu....yaani we acha tu! Leo Man u watatubugiza si chini ya goli 3! maana kila nikicheck kikosi cha Arsenal naona kiza tu
 
Arsenal leo inaingia Old Trafford ikiwa na uhaba wa wachezaji tegemeo saba.

Gervinho, Alex Song, Jack Wilshere, Kieran Gibbs, Emmanuel Frimpong, Abou Diaby na Laurent Koscielny.

Sasa sijui itakuwaje!
 
Hahaha mkuu yeah kwa sasa kikosi chenu sio kizuri kivile ila labda mtashinda kwa nguvu za mwenyezi mungu,na vile vile mpira ni dakika 90 so u never know nini kitatokea au sio??ila bora umekubali kabisa kwamba lazima mnywe leo.......
 
Arsenal leo inaingia Old Trafford ikiwa na uhaba wa wachezaji tegemeo saba.

Gervinho, Alex Song, Jack Wilshere, Kieran Gibbs, Emmanuel Frimpong, Abou Diaby na Laurent Koscielny.

Sasa sijui itakuwaje!

Siku mbaya kwenu mkuu,ila hapo katika list naona wengine umeweka tu kama vibendera, huyo gibbs na diaby hawana madhara hao hata kama wangekuwepo mkuu........labda hapo sana ni huyo song na frimpong
 
Mkuu yaani ni haibu tupu....ukiangalia wachezaji wanatia huruma,ukimwangalia kocha anatia huruma....
wapenzi na mashabiki ndiyo usiseme! washajikatia tamaa na wanatia huruma pia
 
Gibbs na Diaby wanaweza kuanza kwa kukaa benchi maana Armand Traole na Rosicky wanaweza kujaza nafasi zao kwa kuanza. Nafikiri list iliyomaliza game na Udinese ukiondoa Song, ndio itakayoanza leo.

Man U wanaweza kuanza na XI iliocheza na Tottenham Jumatatu iliopita.
 
Ndiyo tushaanza kutapatapa jamani. Alafu habari ambazo ninazo ni kuwa mashabiki wa Arsenal waishio London
wamegoma kwenda old traford japo kuwa walishakata ticket
 
Nimepita mapema kutoa mkono wa rambirambi....bwana alizaa na bwana ametwaa
..jina la Arsenol lihimidiwe...amini.
 
Arsenal leo inaingia Old Trafford ikiwa na uhaba wa wachezaji tegemeo saba.

Gervinho, Alex Song, Jack Wilshere, Kieran Gibbs, Emmanuel Frimpong, Abou Diaby na Laurent Koscielny.

Sasa sijui itakuwaje!

mkuu usijali.. ni soccer mpira unadunda ila reffer akiwa Howard webb ... tuhesabu tushafungwa! jamaa ni mnazi wa man UTD ...

HUYU REFA! NAOMBA ASIWE YEYE

howard-webb_1886372c.jpg

Mkuu yaani ni haibu tupu....ukiangalia wachezaji wanatia huruma,ukimwangalia kocha anatia huruma....
wapenzi na mashabiki ndiyo usiseme! washajikatia tamaa na wanatia huruma pia

Arsene Wenger ameangushwa na madalali na mascout ambao wameshindwa kuja na namba au majina ya wachezaji ambao anataka yeye.

Wenger anataka wachezaji ambao wataziba nafasi ya Fabregas na Nasri yaani playmaking na creativity. Fabregas ni mchezaji creative na Nasri ni playmaker yaani anayumbisha mitindo mbalimbali ya uchezaji ili kuwapa nafasi wengine wafunge -(leo tu amesaidia goli la kwanza la Man City kwa kumtafutia nafasi Dzeko ambae akafunga goli la kwanza).

Fabregas akiwa mbunifu yaani "creative", ana uwezo wa kuona wapi kuna nafasi "Gap" na akaweka mpira hapo na mtu akaweza kufunga na pia pasi zake ni murua yaani "accurate" na ambazo huwa hazipotei.

Sasa Wenger anataka nafasi hizo zijazwe na wachezaji ambao angalau wanafikia uwezo huo bila kupoteza ladha ya mtindo wa uchezaji wa timu hio.
 
Gibbs na Diaby wanaweza kuanza kwa kukaa benchi maana Armand Traole na Rosicky wanaweza kujaza nafasi zao kwa kuanza. Nafikiri list iliyomaliza game na Udinese ukiondoa Song, ndio itakayoanza leo.

Man U wanaweza kuanza na XI iliocheza na Tottenham Jumatatu iliopita.

Nadhani kwa United wataanza na kila kikosi cha last week naona sio kibaya sana na wanacheza mpira mzuri kuliko hata wakubwa zao.....so kwa Arsenal nadhani pressure mtakuwa nayo kwa kipindi cha kwanza na mkiweza kudhibiti then second half kuna uwezekano wa matokeo kubadilika.....zaidi pole sana mkuu
 
Mkuu yaani ni haibu tupu....ukiangalia wachezaji wanatia huruma,ukimwangalia kocha anatia huruma....
wapenzi na mashabiki ndiyo usiseme! washajikatia tamaa na wanatia huruma pia

Hivi huyo kocha anataka mpaka aondoke amewaacha kwenye hali gani???maana sasa hivi wachezaji wa kikosi cha pili ndio anawategemea zaidi ambao bado hawajafuzu kuchezea first eleven.....
 
Arsene Wenger ameangushwa na madalali na mascout ambao wameshindwa kuja na namba au majina ya wachezaji ambao anataka yeye.

Wenger anataka wachezaji ambao wataziba nafasi ya Fabregas na Nasri yaani playmaking na creativity. Fabregas ni mchezaji creative na Nasri ni playmaker yaani anayumbisha mitindo mbalimbali ya uchezaji ili kuwapa nafasi wengine wafunge -(leo tu amesaidia goli la kwanza la Man City kwa kumtafutia nafasi Dzeko ambae akafunga goli la kwanza).

Fabregas akiwa mbunifu yaani "creative", ana uwezo wa kuona wapi kuna nafasi "Gap" na akaweka mpira hapo na mtu akaweza kufunga na pia pasi zake ni murua yaani "accurate" na ambazo huwa hazipotei.

Sasa Wenger anataka nafasi hizo zijazwe na wachezaji ambao angalau wanafikia uwezo huo bila kupoteza ladha ya mtindo wa uchezaji wa timu hio.

Lakini sasa mkuu hao wachezaji watapatikana lini na days zinaisha hivyo??na ina maana mkisema kwamba mbaki na hicho hicho kikosi je kuna uwezekano wa kumaliza top 4??
 
Mimi sina wasiwasi nafahamu huu ni msimu mgumu sana ila lolote linawezekana.

Hapa Tripoli jamaa wa TNC bado wanazungumza na wazee wa Mji wa Sirte ambako Gaddafi amezaliwa ili waweze kuingia kwenye mji huo.

Internet inafanya kazi na bomba la mafuta ambalo linatambaa hadi Italy nao limekwishatengezwa na hawa jamaa.

Jamaa hawa wametangaza majina ya mawaziri ambao wataanza kazi rasmi leo na ni mwanamke mmoja tu yumo humo anaitwa Salwa Fawzi el-Deghali ambae anatoka mji wa Benghazi.
 
Hivi huyo kocha anataka mpaka aondoke amewaacha kwenye hali gani???maana sasa hivi wachezaji wa kikosi cha pili ndio anawategemea zaidi ambao bado hawajafuzu kuchezea first eleven.....
Yaani huyu Wenger kama angekuwa anaishi Bongo basi zamani nishampiga risasi ya kichwa na sasa nahisi ningekuwa Jela
 
Back
Top Bottom