Richard
Platinum Member
- Oct 23, 2006
- 16,667
- 25,695
Uko sahihi kabisa na Fabio Vieira leo ametoa pasi murua sana kwa Jesus kwenda kufunga, na hivyo ndivyo Zinchenko apaswa kuangalia analink vipi mchezo na mchezaji wake wa kiungo (Havertz).Haya masuala ya kumsubiri mtu ajifunze wakati ambao tunataka matokeo ndio jambo ambalo sisi mashabiki hatuwezi kulivumilia.
Kama kuna watu walioko tayari kama Fabio/ESR ni bora muda mwingi wapewe wao huku tukimpa muda kidogo kidogo Havertz wa kujifunza.. awe anaingia time kama zile anazoingia Fabio, dk ya 75 hivi muda huo tukiwa tunaongoza goli 2 na kuendelea au asubiri aanze mechi za Carabao na FA.
Hata mchezaji akiwa mzuri kiasi gani akijiunga na timu ni lazima ajifunze kucheza na wachezaji wenzie wapya mifumo mbalimbali yaani formations.
Kuna kutoa pasi kutoka kwa beki iwe Zinchenko kwa Havertz au Ben White kwa Bukayo Saka na weye kama beki watakiwa ufanye timning ya ile pasi yako na ikiwa mbovu au umechelewa ndo utaona Saka au Havertz ashindwa kuumudu mpira (ball control) na huupoteza kwa adui.
Pia Martinelli na Saka wakiwa wachezaji wa pembeni kuna kujenga mashambulizi na mabeki au Odegaard na kama hakuna hiyo link Arsenal hupata taabu sana kufanya mashmbuliz ya maana.
Hivyo kulink mchezo na mashambulizi hasi kufunga ni lile goli la kusawazisha la Arsenal yaani mchezo umeunganishwa tangia mwanzo hadi mwisho kwa Onana.
Hivyo wenzetu hawa hawauchezi tu mpira na ndo maana Tierney na Tavarez au Lokonga na wamepewa tena muda wa kujifunza namna ya kulink mchezo bila kukimbia tu kama wafukuza sungura wa kitoweo.