Huu hapa mkuu watu hawajui mpira hawajui kwanini tumecheza na 3diamond3
Wanaropoka tu
.

Hii ligi ukitwaa unakuwa bingwa haswa maana unapitia mechi ngumu nyingi sana , hizi alama 3 za leo za Arsenal zimechimbwa haswa

Mikel Arteta alijua kabisa kwamba Steve Cooper atatumia mfumo wake ule ule wa msimu uliopita wa mabeki watatu nyuma , wingbacks ( 3-4-2-1 ) na ndio maana leo Arteta aliamua kuja na mfumo tofauti kama ule ambao Man City walitumia dhidi ya Inter Milan fainali UCL

Tunaita 3-diamond-3 maana yake nyuma mabeki watatu ( White Saliba Timber ) mbele yao namba 6 Partey juu yake namba 8 wawili kulia na kushoto Rice na Odegaard nyuma ya Nketiah kuna Havertz ( wingers Martinelli na Saka ) kwanini huu muundo ?
1: Ili kutengeneza idadi kubwa ya wachezaji katika phase zote tatu ( ulinzi kiungo na ushambuliaji ) hasa wakiwa na mpira , bila mpira ni 4-4-2 haina shida
2: Forest bila mpira walikuwa 5-2-2-1 , shida ilikuwa kwa Gibbs White na Danilo ambao walikuwa nyuma ya Johnson kwamba wafanye nini bila mpira ? Waende kuwapress mabeki wa nje wawili kati ya watatu wa Arsenal ( outside CBs ) White na Timber ?
3: Wakifanya hivyo maana yake viungo wao wawili wa kati ( Yates na Mangala ) wanazidiwa namba inakuwa 3 Vs 2 ( Ode Kai na Rice Vs Mangala na Yates ) lakini wakisema warudi nyuma ( Gibbs White na Danilo ) maana yake White na Timber wanakuwa huru wakiwa na mali
4: Arsenal kwenye phase ya tatu walikuwa wanashambulia na wachezaji 5 mpaka 6 ( Martinelli Nketiah Saka Odegaard Kai na mara kadhaa anaongezeka Rice dhidi ya BACK 5 ya Forest )

Walichofanikiwa Forest hasa kipindi cha pili ni uwepo wa Awoniyi na Elanga , kasi na nguvu maana yake ilikuwa rahisi Forest kufika mbele bila kutumia pasi nyingi bali ni mipira mirefu ns kuokota second balls nyingi . Kuwa jasiri .!
NOTE
1: Johnson atakuwa anawaza alikosaje 1 Vs 1 na Ramsdale ?
2: Saka na Martinelli wanaweza kukutoa damu wale vijana
3: Rice akiwa ana sprint kwenda kuzuia
4: Forest wanahitaji ubora zaidi wa wingbacks kwa mfumo ule
5: Ile assist ya Martinelli
6: MUHIMU ALAMA 3 kwenye mechi ya kwanza
FT: Arsenal 2-1 Notts Forest