Ukisoma uchambuzi wa George ambangile instagram utaelewa leo Mikel kafanya nini ambacho hatukufanya last game ikatucost.
Nimeshindwa tu kuucopy uchambuzi wake.
Huu hapa mkuu watu hawajui mpira hawajui kwanini tumecheza na 3diamond3
Wanaropoka tu
.
[emoji1593]Hii ligi ukitwaa unakuwa bingwa haswa maana unapitia mechi ngumu nyingi sana , hizi alama 3 za leo za Arsenal zimechimbwa haswa
[emoji1593]Mikel Arteta alijua kabisa kwamba Steve Cooper atatumia mfumo wake ule ule wa msimu uliopita wa mabeki watatu nyuma , wingbacks ( 3-4-2-1 ) na ndio maana leo Arteta aliamua kuja na mfumo tofauti kama ule ambao Man City walitumia dhidi ya Inter Milan fainali UCL
[emoji1593]Tunaita 3-diamond-3 maana yake nyuma mabeki watatu ( White Saliba Timber ) mbele yao namba 6 Partey juu yake namba 8 wawili kulia na kushoto Rice na Odegaard nyuma ya Nketiah kuna Havertz ( wingers Martinelli na Saka ) kwanini huu muundo ?
1: Ili kutengeneza idadi kubwa ya wachezaji katika phase zote tatu ( ulinzi kiungo na ushambuliaji ) hasa wakiwa na mpira , bila mpira ni 4-4-2 haina shida
2: Forest bila mpira walikuwa 5-2-2-1 , shida ilikuwa kwa Gibbs White na Danilo ambao walikuwa nyuma ya Johnson kwamba wafanye nini bila mpira ? Waende kuwapress mabeki wa nje wawili kati ya watatu wa Arsenal ( outside CBs ) White na Timber ?
3: Wakifanya hivyo maana yake viungo wao wawili wa kati ( Yates na Mangala ) wanazidiwa namba inakuwa 3 Vs 2 ( Ode Kai na Rice Vs Mangala na Yates ) lakini wakisema warudi nyuma ( Gibbs White na Danilo ) maana yake White na Timber wanakuwa huru wakiwa na mali
4: Arsenal kwenye phase ya tatu walikuwa wanashambulia na wachezaji 5 mpaka 6 ( Martinelli Nketiah Saka Odegaard Kai na mara kadhaa anaongezeka Rice dhidi ya BACK 5 ya Forest )
[emoji1593]Walichofanikiwa Forest hasa kipindi cha pili ni uwepo wa Awoniyi na Elanga , kasi na nguvu maana yake ilikuwa rahisi Forest kufika mbele bila kutumia pasi nyingi bali ni mipira mirefu ns kuokota second balls nyingi . Kuwa jasiri .!
NOTE
1: Johnson atakuwa anawaza alikosaje 1 Vs 1 na Ramsdale ?
2: Saka na Martinelli wanaweza kukutoa damu wale vijana [emoji91]
3: Rice akiwa ana sprint kwenda kuzuia [emoji91]
4: Forest wanahitaji ubora zaidi wa wingbacks kwa mfumo ule
5: Ile assist ya Martinelli [emoji91]
6: MUHIMU ALAMA 3 kwenye mechi ya kwanza
FT: Arsenal 2-1 Notts Forest