Pepe sio kweli Arteta hanihitaji -
"Watu wanasema kwamba alinitambua kama mchezaji ambaye hakuwa katika kiwango cha timu yake, katika falsafa yake. Ni uongo kabisa. Alipofika, alikuwa na falsafa ya City. Huko walikuwa na kikosi kilichojaa ubora katika kila nafasi."
"Alipoongea na mimi alisema ananitegemea, alitaka nifanye hiki au kile, na wewe uzingatie lile, aliniboresha kwa kila jambo. Aliongea nami muda wote, natazama video na wasaidizi wake wakati wote. Aliniamini sana. Alisema nina uwezo wa ajabu, kwa hiyo tunahitaji kuutoa uwezo huo,”
“Msimu wa kwanza ulipoisha, alizungumza na mimi na kuniambia nifanye hiki au kile, msimu wa pili unakuja, nilikuwa mbadala, nilikuwa nikichanganyikiwa, ningewezaje kuwa mbadala wakati alisema ananiona Nina uwezo, Nilikuwa mbadala wa mechi 10.
"Ilikuwa wakati huo walipomsajili Willian. Yeye ni namba 10 au winga. Lakini alicheza winga kama mechi 11 au 12 mfululizo. Kichwa changu kilivurugika nikijua kuwa niliyozungumza na kocha haikuwa hivyo.” “Lakini hilo liliimarika kwa maana alinipa nafasi, nilifunga dhidi ya Sheffield United pale Emirates.
Kujiamini kulianza kurudi. Nilianza kuongea na mawakala, lakini hatukuonana kama hapo awali.
Sio kweli kwamba hakunihitaji Alinisaidia kwa kila njia, kwa kiwango cha mbinu, katika suala la akili ya mchezo kwa sababu falsafa yake inahitaji akili nyingi. Alijua uchezaji wangu haukuwa unasubiri kumiliki mpira, ulikuwa wa kuingia ndani, haukungoja kulia tu"
"Hapo awali huko Lille nilikuwa huru zaidi. Ilinibidi kusubiri mpira katika eneo langu, na sikuwa hivyo hapo awali. Hizi ni sehemu za mchezo wangu ambazo alijaribu kuboresha. Kila mara alitaka kunisaidia kwa hayo yote."