Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Hivi unaweza ukajiita shabiki wa mpira halafu unashabikia man city??
Kama wewe ni shabiki wa city utulie tu unajichoresha
 
Arteta angepiga chabo hata kwa Morinho na Fergie jinsi ya kucheza mechi za mwisho mwisho,hizi mechi za mwisho lazima utumie mda mwingi kwenye defence.
Hiki kitu nilikuwa nawaambia raia hapa nyumbani kwangu, game za mwisho wa msimu huwezi kuziendea kichwakichwa wakati kila team inawaza kumaliza ligi vizuri. Ni lazima uziendee na mpango kazi wa kutafuta magoli mapema kisha uyalinde haswa.


Bado hamjakutana na Newcastle ambae anaitafuta top four kwa udi na uvumba na anaona kila dalili za kuipoteza baada ya kufungwa mechi yao iliyopita, bado Man City mwenyewe na nyingine nyingi tu ambazo zitakuwa ngumu.
 
Daaah msimu uliopita top 4 tuliikosa hivi hivi kwa game za mwisho . Msimu huu ubingwa nao tumeukosa kindezi sana.
Huwezi ukawa unagombania ubingwa halafu hapo hapo una drop points kwa game ambazo ulikuwa unaongoza kwa goals margin ya 2 daah yani ni utoto wa hali ya juu .

Ubingwa tusahau tena kama mwaka huu tumeshautupa kwa city tayariii . Westham na liverpool wote walicheza midweek games bado tumeshindwa kuchukua points kwao. Ujinga huu unaukuta kwa arsenal tu hata leicester , man utd , chelsea , na wengine wangekuwa kwenye position kama yetu wasingefanya upumbavu huu, its only kwa arsenal tu vitu kama iviii ndo hutokea na si timu nyingine .
Arsenal ni timu inayotoa false hope miaka nenda rudiii toka 2004 mashabiki tunapewa false hope .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…