Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Sisi Westham leo ndio tunaanza rasmi mbio za kusaka nafasi ya kucheza mashindano ya ulaya msimu ujao, tolekaaaa.
 
Hebu niambie, Newcastle plan not to extend Maximin contract after the end of the season,
Technically huyo dogo anakosa nini mbona namuona ndiye star pale Newcastle? I wish angekuwa kwetu asaidiane na flanks zetu. Is it for his injury record?
Maximin kuna vitu inabidi aviongeze, kuna vingi anakosa,inabidi apate mwalimu mzuri amtulize atulie atakuwa mchezaji mzuri.

Maximin ni kama nzi akitulja vizuri anaweza kutoa asali.
 
Hebu niambie, Newcastle plan not to extend Maximin contract after the end of the season,
Technically huyo dogo anakosa nini mbona namuona ndiye star pale Newcastle? I wish angekuwa kwetu asaidiane na flanks zetu. Is it for his injury record?
Dah akija utamchukia.

Ni aina ya mchezaji ambaye anaenjoy kukaa na mpira, kutoa pasi au kuungana na wenzake katika counter kwake ni ngumu.

Timu ngapi za top 4 zina mchezaji kama Maximin? Unadhani hawamuoni? Sisi Pepe tuliachana naye kwaajili hiyo
 
Mfumo wa
FRANSIS CAGIGAO: JINSI NILIVYOMPATA MARTINELLI

Na hamis77

Fransis Cagigao Skauti wa muda mrefu wa Arsenal ,amedumu kwa miaka 24 had mwaka 2020 alipoondoka Arsenal .Amefanya kazi na Arsene Wenger,Unai Emery na Mikel Arteta.

Huyu ndiye Skauti aliyewaleta Nyota wengi waliopita Arsenal ,

Kama ulikuwa hujui Basi hawa Nyota Ni Jicho lake katika kushawishi bodi na benchi la ufundi waletwe Arsenal

Wachezaji hao Ni Lauren Maya, Cesc Fabregas, Jose Antonio Reyes, Santi Cazorla, Nacho Monreal, Mikel Arteta, Emiliano Martinez, Granit Xhaka, Alexis Sanchez, Carlos Vela, Hector Bellerin, Robin van Persie

Mwisho kabla hajaondoka Arsenal akatuachia zawadi ya Gabriel Martinelli na William Saliba.


Leo nitaelezea jinsi alivyompata Martinelli katika kazi yake ya Skauti ,huyu alikuwa ndiye HEAD OF SCOUTING PALE ARSENAL

Huyu ndiye aliiambia bodi ya Arsenal itoe €30m kwa kijana mdogo miaka 18 ,William Saliba mwaka 2019 ,Bodi ya Arsenal ilisita Sana mwisho ilikubali ushauri wake


Leo nakuletea Simulizi jinsi alivyomuona na kumleta Gabriel Martinell ndani ya Arsenal mchezaji ambaye alikataliwa Manchester United mwaka 2018.

Anasema Francis Cagigao" Nilienda kuangalia mechi Hakuwa na mechi bora zaidi. Alitolewa baada ya dakika 70. Lakini hakuwa na hofu. Unaweza kuona kwamba ingawa mambo hayakuwa sawa kwake. Alikuwa akitengeneza nafasi, anakimbia , Alikuwa na mwendo kasi, ukakamavu - hangesukumwa nje ya mpira, hapo ana umri wa miaka 17. Ufundi wake haukuwa mzuri lakini alikuwa na sifa ambazo Nilisema: "Ninampenda. Je, tunaweza kumleta kwa mazoezi ya wiki moja Arsenal?"


. Ituano hawakutaka Martinelli aende kwa majaribio ya wiki moja huko Arsenal, jambo ambalo halikuwa la kawaida, kwani ada ya uhamisho kutoka kwa timu za juu za Ulaya kwa kawaida inatosha kwa vilabu vya Amerika Kusini kuwakaribisha vijana wao kwenye chumba cha kupumzika. Siku kadhaa baadaye, Cagigao alisikia kwamba Martinelli alikuwa ameenda Barcelona kwa majaribio ya wiki moja badala yake. ‘Nilifikiri ningempoteza,’ asema Cagigao. Kwa kupendeza, kwa mtazamo wa Arsenal, Martinelli pia angetumia wiki mbili tofauti Manchester United. Walimtuma apakie, pia Barcelona. Cagigao alikuwa amerudi kwenye ndege. Alikumbuka: ‘Niliwaambia maskauti wangu wote: “Wekeni kalamu zenu chini, nataka kila mtu anayemtazama mvulana huyu kwenye video.” Nilitaka kila mtu amuangalie , Kwa nini? Kwa sababu alikuwa mchezaji wa daraja la nne wa Brazil!

Tulikuwa na Kitengo cha takwimu na uchambuzi Arsenal lakini katika mpango huu wa kumsajili Martinelli, hatukufanya kazi na takwimu. Wakati wa kutathmini vipaji chipukizi, hakuna mbadala wa jicho la mafunzo, mchezaji wa zamani au kocha ambaye ana akili ya uchambuzi."

Sikutaka watu waseme: “Francis , umemtoa wapi bila kutushirikisha! Nini kinaendelea hapa?” Nilitaka niweze kusema: “Hapana, si mimi tu ninayesema.”’ Wakati huu ilikuwa mwendo wa saa mbili kwa gari hadi Ituano ambako Ituano anacheza. Uwanja si mkubwa ,unachukua watazamaji 18,000 na una paa moja tu. Hupati wanasoka wengi wa kiwango cha kimataifa hapa, ingawa Juninho wa Middlesbrough ni rais wa klabu na alianza katika akademi. Lakini hakuna hata mmoja wa wakubwa wa Sao Paulo ambaye alikuwa amemwona Martinelli pale Ituano.

Ila kwa sasa kila mtu alijua Cagigao kwa nini alikuwa huko. Rafiki wa familia ya Martinelli alikuwa ametoa nyumba yao kwa Cagigao kwa kikao na Gabriel na baba yake mzee Joao . Lakini alipofika Cagigao anakumbuka kulikuwa na maajenti wengine 10 ndani ya nyumba.

Nilisema: "Bila ushawishi wakuongea Basi nitajikuta narudi London peke yangu".

Mwishowe baba na Gabi walisema: "Tutazungumza peke yetu".

Sijawahi kuwa na mkutano na mchezaji na familia yake kwa kushawishi kama huo, tangu nilipofanya hivo kwenye kumleta Cesc Fabregas Arsenal akiwa na miaka 16.

‘Walikuwa watu wenye kipaji, wanyenyekevu, watu wa hali ya chini(masikini). Mtoto alikuwa mwenye akili, anayehusika kwenye kikao na msikilizaji mzuri. Baba alikuwa akisema: "Angalia Francis, ni maisha ya Gabi.

Gabi bora ajibu maswali mwenyewe kuhusu kwenda Arsenal. Sitaki aje akisema kwamba niliharibu maisha yake”. Na Gabi alitaka kuzungumza juu ya mpira wa miguu, mchezo wake. Alikuwa mwanafunzi anayeelewa haraka, ambacho ni muhimu siku hizi.

Mkutano juu kukamilisha dili ulinifanya nitoke nje na kumpigia simu Raul Sanllehi, ambaye wakati huo alikuwa mkurugenzi mkuu wa Arsenal] na kusema:

“Sina shaka. Kijana huyu atakuwa mchezaji bora. Hebu tumsaini kwa Hiyo Pesa”.

Ada ya £4m ilijadiliwa. Wakati Cagigao alikuwa amerejea London ilipanda hadi £6m

Arsenal ililipa £6m na Martinelli akajiunga Arsenal









View attachment 2589745
Mfumo wa soka la brazil ni mzuri saana, ituano ilikuwa ligi daraja la nne kipindi hicho, lakini bado ilikuwa inacheza ligi ya jimbo.

Mfano hapa daslam kuwe na ligi ya mkoa, abajalo ya daraja la 3 ki nchi lakini inacheza na kina simba,kmc, yanga, azam n.k kwenye ligi ya mkoa.
 
Back
Top Bottom