Salamu wakuu.....Poleni sana Gunners wenzangu kwa msimu mbovu tuliokuwa nao,maana hali ilikuwa mbaya hasa mechi za mwisho,zingeingezwa mechi 3 ama 5 zaidi tungeumbuka,tungeweza hata kushika nafasi ya 7 kama sio ya 6......Tukeshe tukiomba ili AW aondolewe Arsenal,hana jipya,kaishiwa,tunahitaji meneja mwingine......
Hongera sana kwa watani Manda,Belo,Eqlypz,Idimi,Belinda Jacob,Mfarisayo na Red Devils wengine kwa kuchukua ubingwa wa EPL....Hakika mlistahili kuwa mabingwa....Nawatakia kila la heri katika mechi yenu ya kesho kutwa ya fainali ya UCL.....Nawaombea muwachape Barca 'wazee wa kubebwa'.....Tuko pamoja katika hili,nina hakika ubingwa ni wenu watani wangu....
Ombi kwa Eqlypz na mods wengine,kuna mtu anaitwa Rutashubanyuma,naona kaamua kuvamia kwenye majukwaa yetu na 'copy and paste' zake kwa kasi ya ajabu.......Habari zenyewe za magazeti anazoleta anafanya double posting hivyo kutujazia tu bandwith.....Si vibaya akawa anaweka links tu ama azipeleke habari hizo kwenye ile thread yake ya michezo magazetini