BEN WHITE
Msimu huu kwa " baadhi " ya mashabiki wa Arsenal wachezaji ambao wapo kwenye mawazo na midomo yao sana ni Saka, Odegaard , Martinelli , Partey , Zinchenko , Saliba , G.Jesus lakini kuna jina inawezekana ukakutana na wana " Gunners " kumi lakini wasilitaje : BEN WHITE
Binafsi naamini ukitaja wachezaji wanne muhimu wa Arsenal msimu huu nitataja jina la Ben White nikiambatanisha na sababu zangu ambazo ni :-
1: Upatikanaji wake uwanjani . Sikumbuki lini nilisikia Ben White atakuwa nje ya dimba kwa miezi kadhaa au wiki 3 . Moja ya sifa kubwa kwa mchezaji bora ni upatikanaji wake
2: Kutoka kuwa beki wa kati mpaka beki wa kulia na kucheza hiyo nafasi utasema ndio ulianzia huko maisha yako ya soka sio rahisi hata kidogo . Binafsi naamini ni nafuu kuwa beki wa pembeni kucheza beki wa kati kuliko wa kati kuwa fullback
3: Ben White amekuwa muhimu sana katika muundo wa uchezaji wa Arsenal na ana husika katika phase zote tatu . Kuna wachezaji ambao wanahusika :-
A : Kwenye phase ya kwanza pekee ( kuanzisha mpira nyuma ) build up
B: Phase ya pili pekee ( kwenye kiungo )
C: Phase ya tatu pekee : kwenye ushambuliaji
Lakini Ben White ndani ya Arsenal anatumika kwenye phase zote tatu ... kivipi ?

Arsenal wakiwa na mpira White anabaki nyuma kutengeneza BACK 3 ( White Saliba na Gabriel ) ili kumruhusu Zinchenko kuingia ndani kama kiungo karibu na Partey kwenye muundo wa 3-2-2-3

Arsenal wakisogea juu Ben White anakuwa kama msingi wa Bukayo Saka na Odegaard ule upande wa kulia wa Arsenal ( Odegaard kama namba 8 wa kulia , Saka winger na White anakuwa nyuma yao .

Wakifika eneo la wapinzani Ben White anakuwa mara nyingi mpishi wa Saka kwa kupiga pasi za ndani zaidi ni mara chache kumuona White anafanya overlaps
Kuna hili sasa la muhimu sana : waangalie Arsenal wakiwa na mpira na position ya White : kwenye ile " REST DEFENSE " ya Arsenal ( Yani namaanisha shape yao ya ulinzi wakiwa wanashambulia ) yeye anakuwa sambamba na Zincheno Partey na White katika mstari mmoja compact mbele ya Saliba na Gabriel wakiwa tayari kuzuia counter attacks lakini pia kupora mpira na kuurejesha kwa watu wa mbele ( recycle possession to sustain attacks )