Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kuna manyumbu huko mtanaoni wanalalamika eti Rashford yuko wapi?

We timu imepigwa 7-0 halafu waweke mchezaji wao, hawa nyumbu hawana wazimu kweli!?
Manjesta utd mwezi huu MARCH EPL ndio timu pekee hajafunga goli hata moja katika michezo yake yote pia wana aggrigate ya goli 7
 
Ikiwa record ya kushinda ukocha Bora wa mwezi katika EPL ndani ya msimu mmoja ikishikiliwa na Jürgen Klop akiwa kashinda mara 5

Super Mikel anaenda kujaribu Ku challenge record ya Klop kwani teyari anazo tuzo 3 katika msimu huu, na mwezi huu pasina Shaka anaenda kuchukua tuzo ya 4 ya kocha Bora mwezi wa 3

Sasa je, katika mwezi wa 4 na 5 ataweza kupata tuzo zingine ili afikishe 5 na hatimae kuwa sawa na Klop au kumpita kabisa?
View attachment 2562750
Hapa hata Mimi nyumbu nimempigia arteta maana kwa mwezi uliopita japo Ulikuwa na mechi chache lakini kafanya vyema.
 
dah hata kama ni Nyumbu ila ukweli unauma tunaupokea
Inaonyesha kwa uwanjani mmeshindwa kulipata fanyeni mpango mliibe basi.
20230307_091251.jpg
 
Hapa hata Mimi nyumbu nimempigia arteta maana kwa mwezi uliopita japo Ulikuwa na mechi chache lakini kafanya vyema.
Japokuwa waga ni mara chache sana kuona Nyumbu anaelekea uelekeo ulio sahihi ila hapa nakupa big up maana upo sahihi

Mikel mwezi wa 3 amekichafua sana, na hasa ile game ya Bournemouth ya kutoka 2 bila hadi 3-2, hiyo Tu inatosha kumpa ukocha bora wa mwezi
 
Tunazungumzia EPL kijana, hayo mashindano mengine kina Reading, chalton ,Forest home and away ,

Martinell hajafikisha mechi 41 kijana , usidanganye
Kwhy uwezo wa mchezaji unapimwa kwa kuangalia EPL, Pekee.??
Mechi alizocheza kwenye Mashindano mengine kama World Cup etc hazihesabiwi??

Na kama unahisi mimi nadanganya Martinelli hajacheza mechi 41 msimu huu kwenye mashindano yote.
Basi nambie wewe kacheza mechi ngapi.
 
Mkuu Rashid msimu huu yupo vizuri, yupo katika kilele cha uwezo wake, hatujui tu kuhusu consistency kama itakuwepo
 
Arsenal fans hatumpi Martinelli heshima anayostahili , ona kelele za Manjesta kina Ally pipi Wanataka Rashford apewe Ballon dor ,Cha ajabu amemzidi Nelli goli 1 na Nelli atamaliza juu ya Huyo Rashidi,

Swore the way united fans talk about Rashford it’s like he was on 25 goals or sum and he’s only one above martinelliView attachment 2562742
My nigga Toney, shows what he is capable of.
 
Wakati tuzo ya kocha Bora wa mwezi ikitegemewa kwenda katika viunga vya Emirates

Huku nako katika tuzo ya mchezaji bora wa mwezi inategemewa kwenda kwa Bukayo Saka Kwa mara ya Kwanza katika msimu huu

Akiwa kahusika na magoli 3 na assist 2 katika jumla ya mechi 4 alizocheza mwezi March, anatazamiwa kupata tuzo hii japokuwa atapata ushindani kutoka kwa Trossard,Isak pamoja na Salah

Pamoja na hayo ila kumekuwa na lawama kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa Arsenal wakisema Martinel hajafanyiwa fair kwa kutokuchaguliwa katika kinyang'anyilo hicho, kwani katika mechi 4 bwana mdogo amefunga magoli 4View attachment 2562762
Wameona aibu kuweka players watatu wa arsenal FA bna
 
Wameona aibu kuweka players watatu wa arsenal FA bna
Rashford alifunga Goli 2 mwez uliopita wakamuweka na tuzo wakampa

Martinell ana Goli 4 mwezi huu Cha ajabu hata kwenye nominees hayupo

Mashabiki wengi wa Arsenal wameanza kupaza sauti usishangae asiwekwe hata kwenye Nominees ya YOUNG PLAYER OF THE YEAR na ana miaka 21, akawekwa Rashford anayetafuta mwaka wa 27

Tunasema haya ,msimu uliopita Saka kadhulumiwa tuzo nyingi tu
 
BEN WHITE

Msimu huu kwa " baadhi " ya mashabiki wa Arsenal wachezaji ambao wapo kwenye mawazo na midomo yao sana ni Saka, Odegaard , Martinelli , Partey , Zinchenko , Saliba , G.Jesus lakini kuna jina inawezekana ukakutana na wana " Gunners " kumi lakini wasilitaje : BEN WHITE

Binafsi naamini ukitaja wachezaji wanne muhimu wa Arsenal msimu huu nitataja jina la Ben White nikiambatanisha na sababu zangu ambazo ni :-

1: Upatikanaji wake uwanjani . Sikumbuki lini nilisikia Ben White atakuwa nje ya dimba kwa miezi kadhaa au wiki 3 . Moja ya sifa kubwa kwa mchezaji bora ni upatikanaji wake

2: Kutoka kuwa beki wa kati mpaka beki wa kulia na kucheza hiyo nafasi utasema ndio ulianzia huko maisha yako ya soka sio rahisi hata kidogo . Binafsi naamini ni nafuu kuwa beki wa pembeni kucheza beki wa kati kuliko wa kati kuwa fullback

3: Ben White amekuwa muhimu sana katika muundo wa uchezaji wa Arsenal na ana husika katika phase zote tatu . Kuna wachezaji ambao wanahusika :-

A : Kwenye phase ya kwanza pekee ( kuanzisha mpira nyuma ) build up

B: Phase ya pili pekee ( kwenye kiungo )

C: Phase ya tatu pekee : kwenye ushambuliaji

Lakini Ben White ndani ya Arsenal anatumika kwenye phase zote tatu ... kivipi ?

Arsenal wakiwa na mpira White anabaki nyuma kutengeneza BACK 3 ( White Saliba na Gabriel ) ili kumruhusu Zinchenko kuingia ndani kama kiungo karibu na Partey kwenye muundo wa 3-2-2-3

Arsenal wakisogea juu Ben White anakuwa kama msingi wa Bukayo Saka na Odegaard ule upande wa kulia wa Arsenal ( Odegaard kama namba 8 wa kulia , Saka winger na White anakuwa nyuma yao .

Wakifika eneo la wapinzani Ben White anakuwa mara nyingi mpishi wa Saka kwa kupiga pasi za ndani zaidi ni mara chache kumuona White anafanya overlaps

Kuna hili sasa la muhimu sana : waangalie Arsenal wakiwa na mpira na position ya White : kwenye ile " REST DEFENSE " ya Arsenal ( Yani namaanisha shape yao ya ulinzi wakiwa wanashambulia ) yeye anakuwa sambamba na Zincheno Partey na White katika mstari mmoja compact mbele ya Saliba na Gabriel wakiwa tayari kuzuia counter attacks lakini pia kupora mpira na kuurejesha kwa watu wa mbele ( recycle possession to sustain attacks )
 
Cc. Mwalimu George Ambagile...! Jamaa ni miongoni mwa wachambuzi wachache sana Duniani achilia mbali Tanzania ambao kipindi Arsenal iko Hoi bin Taaban chin ya Arteta yeye alikuwa anasimama na Mikel

Alikuwa anasema kuna kitu anakiona ndani ya Arsenal kinasukwa na ni swala la Muda tu watu watakuja kukiona, na hatimae leo hii wengi waliokuwa wanamkataa Arteta wamemkubali
 
Back
Top Bottom