ARSENAL VS CRYSTAL: KUTAWAKA MOTO 🔥
Tunasonga mbele na kusahau kilichotokea, tunafungwa pamoja na tunashinda pamoja
Emirates, London... kutawaka moto majira ya Saa kumi na moja (kwa Afrika Mashariki), Washika Bunduki wakiwa karibisha Tai wa London, Hii ni London Derby haswa. Ukiwa ni mchezo wao wa 26 tangu Vilabu hivyo Viasisiwe.
Katikati ya Wiki, Crystal Palace walitangaza Kuachana na aliyekuwa Kocha wao Patrick Vieira tokana na mfululizo wa matokeo mabovu... jahazi likiwa mikononi mwa Nahodha wao wa Zamani na Kocha wa Kikosi Chao cha U-21, Paddy MCcarthy , hadi watakavyo amua Vinginevyo.
Akiingia na tahadhari ya Kumkosa Kiungo Albert Sambi Lokonga ambaye Kwa Sheria za England hawezi kucheza na Waajili wake kwani yupo kwa Mkopo. Kipa Guetta, Will Hughes na James Mc Arthur wapo mashakani kucheza Mchezo wa Leo
Ama Arsenal Wao watamkosa Beki William Saliba, Huku Eddie Nketiah na Takehiro Tomiyasu wakiwa katika hati hati. Huku taarifa ya Kuitwa Kikosi cha Kwanza Reuel Walters ikipokewa kwa hisia mbali mbali.