Naangalia mechi halafu nakumbuka miaka miwili nyuma nilivyokua nasema timu imejaa wachezaji hawana fighting spirit, hawana morali, wanapiga sideway passes n.k.
Sasa hivi naangalia mechi, tunafungwa goli moja na ninaamini tunaweza kufanya comeback na tunafanya kweli. Odegaard kwa pesa tuliyolipa ni tumemuiba, Nketiah is scoring yes lakini naona tunahitaji zaidi ya hiyo, why? Akipata mpira na kwenda mbele hana agility na skills za kuchambus defense, Jesus ana hivyo viwili ndiyo maana anaweza asiscore ila akatoa assists au akawa chanzo cha goli.
Tusiwasikilize wakina Ollashoga na Lembua. Walitoa vipimo vingi mara hatutapona kwa huyu au yule na stori zikahamishwa mpaka kudai baada ya WC tutakua hovyo.
Well baada ya WC tumeshinda mechi ya pili, ukiniuliza mimi nitasema nina hamu na game dhidi ya City kwakua ni miongoni mwa timu zilituburuza na ninataka kuona tumefikia wapi. Hawa wengine hawanisumbui.
Happy New Year Crew