Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Yaani kuongoza ligi kwa points 3 dhidi ya Man U ni kama mko sawa ndio yale yale ya Chelsea msimu uliopita ni swala la muda tu mtatoka hapo juu na mtapoteza kujiamini maana wachezaji wenu wengi ni watoto.
Wewe usifananishe Chelsea na matakataka wewe kuwa adabu
.timu inafungwa hadi na ingizo jipya munakuja kuifananisha na mabingwa wa Dunia.?!
 
ulitazama mech mkuu?

Nilitazama mechi mkuu.

Xhaka na Odegaard kiushauri sio wa kusema una midfielders wa kupambana na Club vigogo

Fikiria kipindi Real Madrid Modric ana umri wa miaka ishirini na kitu hapo hapo yupo na Kroos ,hali kadhalika Barca kipindi Xavi ,Iniesta na Busquets wana miaka ishirini na kitu leo hii Arsenal inategemea Xhaka na Odegaard wakiwa wanaanza kwa pamoja
 
Thomas Partey ndie anchorman pale kati na yupo anarudi mambo yatakuwa sawa.

Xhaka hucheza uzuri akiwa na Partey kuliko akiwa na Lokonga.

Odegaard wamuonea kwani yeye ni creative Midfielder na leo kacheza bado akiwa hayuko fit, maana aliumizwa kwenye mechi na Aston Villa.
 
Wapenzi wa Arsenal twaamini safari hii lazima timu faulu kucheza CL.

Hiyo ya Ubingwa si priority kwani ni mapema mno kuzungumzia ubingwa.

Ubingwa huangaliwa baada ya 20 games.

Game 19 Mkuu,hapo ndio utakuwa umecheza na kila timu lakini game 6 peke yake utakuwa kuna baadhi ya timu ujacheza nazo wenzako wamecheza nazo kwa hiyo wewe umependelewa kwenye ratiba lakini 19, kila timu utakuwa umecheza nazo.

Ndio maana wanasemaga December ukiwa juu utakuwa bingwa lakini tafsiri yake ni mechi 19, zinakuwa zimefika kuna muda itakuwa December imefika lakini bado mechi ni 15 sasa subiria mpaka 19 ,timu zinakuwaga na viporo.

Ndio maana tunaona Liverpool yuko juu December lakini ubingwa anaukosa mechi bado zinakuwa bado raundi kuisha unakuta mechi ni 15 tu sasa hapo bado timu 4 ajacheza nazo.
 
Ode hakuna na kitu kipya tena leo naweza kusema ndo katukosesha ushindi, kuna eneo la kushoot ndan ya 18 anatoa pasi za ovyo ovyo, kwa jinsi alivyoingia Viera na kucheza vile Ode ajiangalie sana
 
Manchester united wana kocha mzuri na mwenye mbinu,tatizo la Arsenal bado ni ubahili mkuu,hatuna wachezaji wa kushindana na timu hata hivyo wanajitahidi sana
 


Mkuu wangu Richard Odegaard nimemuangaliaga sana sana ila sijawahi kumkubali sana any way nampa benefit of doubt
 
una hoja mkuu.na hili kuna namna limetugharimu kiasi chake.ila linafanyiwa kazi.mpira ni structure na inatengenezwq
 
kwako changes ni kuifunga man u pekee?
Top 6 imagine tunalose vs Rashford itakuwaje Vs Halaand Vs Salah Vs Kane Vs Auba? We need to win vs Top 6 teams but limeshindikana hili suala may be katika 10 games Vs Liverpool Manchester City Manchester United Chelsea Spurs may be may be we are going to win 2 out of 10 games



Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Tena tunakuja kuchukia haraka maana hawana nidhamu Hawa wahaini.mechi 5 wanajitangaza mabingwa

Hawatafika kokote hao yaani kelele kibao saizi wamewazidi Man U points 3, hapo kama wako sawa na Man U tu,muda wowote kibao kina badilika.

Hao wengine Vipi walioposhana point moja?
 
Mkuu wangu Richard Odegaard nimemuangaliaga sana sana ila sijawahi kumkubali sana any way nampa benefit of doubt
Odegaard akiwa fit ni mchezaji mzuri na ndie aliisaida sana Arsenal mechi tano za kwanza.

yeye ni Creator na hufungua vyumba sana.

Ila leo kachezeshwa tu bado hayupo fit.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…