Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Leo nipo na arsenal bega kwa bega...wakuu msiniangushe..mkishindwa kabisa ata sare tena ya magoli...si tupo nyumbani kwetu #WashikaMitutu!!!
Dah!...kiuhalisia arsenal mnacheza vizuri kuanzia beki hadi kiungo wanaelewana vizuri tu...ila shida ni kule mbele mkikutana na timu kubwa mnakosa zile clinical finishing.

ITOSHE KUSEMA KUWA...UWEZO WENU NDIPO ULIPOISHIA PALE.

TULIWAPA KAZI YA WANAUME TUKISAHAU NYIE NI WAVULANA, SASA SISI CITY KAZI YA KUMTULIZA LIVERPOOL TUTAIFANYA WENYEWE APRIL-10.
 
Nilishauri mapema leo tutizame gem yetu kwa kuwafuatilia wachezaji wetu ambao huwe tunawabishania ambao mara nyingi ni Xhaka na Gabriel. Nadhani mwenye kuona ameona kazi ya Gabriel na pia ameona kazi ya Xhaka. Swali ni je Xhaka ni moja ya viungo wasiyohitajika Arsernal? Na je kulingana na mtizamo wa will jr ni kweli kuwa tunahitaji kuwa na akina White wawili kuliko kuwa na White na Gabriel?.

Tangu Arsenal ya zama za wenger ambayo wengi wetu tumeishuhudia vzr huwa inashindwa kuhimili timu zinazotumia nguvu na kasi(fujo) na hata huwa tukijaribu kupambana bado kuna wachezaji wetu huwa wanapotea kwenye gem na hii mara nyingi nadhani ni tabia ya wafaransa kwan hata ukifuatilia timu yao ya taifa huwa unapata tabu sana kwa mataifa yanayotumia nguvu na kasi kuliko yale yanayochezea mpira. Kwahiyo kwa mtazamo wangu naona hilo pia Arteta alifanyie kazi.

Leo tumecheza vizuri hasa kwenye eneo la kiungo ambapo Xhaka na Partey walionekana kweli wao na seniors lkn kwa wale ambao huwa tunawategemea kuturahisishia kupata magoli(Odegaard & Saka) leo gem imewashinda na ni kwa sababu ya matumizi ya nguvu kwa mpinzani.

Tulimuhitaji Rowe na Pepe mapema zaidi ili kuupa nguvu upande uliokuwa umeelemewa(upande wa kulia) kwa kuwa Rowe anatabia ya kukimbia kwenda mbele na Pepe ana nguvu, speed na anaweza kutoka kwa mabeki zaidi ya 2

Sioni sana shida ya Lacazette maana sio 9 wa kusimama na mara nyingi arteta amekuwa akimfanya Lacazette acheze km 10 na kuacha eneo la ushambuliaji likiwa wazi ili pale timu inaposhambulia unakuta viungo au washambuliaji wa pembeni wanaingia kwenye lile eneo na kufunga kiurahisi na ndo maana utakuta magoli tunayofunga Lacazette anakuwa ameshiriki.



 
Shida yenu humu mna hesabu mayai ambayo kuku hajataga mpira ni matokeo siku zote mtabaki kusema mmecheza vizuri kila siku wenzenu wanaondoka na point 3
 
Bonge la game ....Mimi naona arsenal kacheza poa ...kiufupi ndio level zake

Kila mbuzi atakula kwa urefu wa kamba yake
 
Arsenal imekuwa inashida kubwa Sana na imeendelea nayo mpaka msimu huu mmekuwa vibonde wa team kubwa Sana kazi yenu nikuwaonea wadogo tu na kumbukeni mnakipolo Cha mwisho ambao ni Chelsea kama kawaida yenu mjiandae nakuacha point 3 mezani
 
Middlesbrough have announced they will be selling Chelsea's ticket allocation for Saturday's FA Cup clash to their own fans.
-sky sports

vita mbaya sana

so inamaana mashabiki wa chelsea hawataweza kununua tickets unless ni wale season ticket holders, so Boro waliombwa wawasaidie kwa kuuza baadhi ya zile ticket zilizotengwa kwa mashabiki wao kwa mashabiki wa chelsea ili angalau wapate balance ya mashabiki?
Vikwazo wanawekewa Chelsea. Madhara yanatokea kwa Arsenal na Man U. Poleni sana
 
Back
Top Bottom