Nimeshtuka sasa hivi nimeingia sofascore nimekuta 0-0.
Mzee wangu ni mwanajeshi mstaafu aliwahi kuniambia kwamba anaamini ubora wa mwanajeshi ni katika kutumia silaha ya kawaida aliyonayo ili iwe na madhara kuliko mwenye silaha advanced.
Ilikua tunaongelea jinsi Tz tumeachwa nyuma hata na baadhi ya nchi za Afrika kijeshi.
Nikikumbuka alichosema nikiiangalia Arsenal na Villar nafikiri kilichoipitisha Villar ni uwezo wa kocha zaidi kuliko wachezaji ilionao.
Na hata sisi tulivyofika fainali Europa chini ya Emery ilikua ni uwezo wa kocha zaidi kuliko hata kikosi, kama mnakumbuka Europa ST alikua anapangwa hadi Nketiah na matokeo tunapata. Leo Arteta anakuambia last minute changes na kulazimika kumpanga Tierney ambaye hana mazoezi lilikua ni tatizo lililotunyima ushindi ila huyu Tierney ndiye alishirikiana na Gabriel chini ya Emery tukawa tunafunga watu 5, 4 goli chache 3.
Haya sawa, Xhaka kaumia, kwani Saka hajawahi kucheza LB kwanini asipangwe yeye ambaye yuko fit kumzidi Tierney? In fact Saka kua LB kunakupa gape ya kumpenyeza Martinell kule mbele. Means utakua na watu watatu ambao wanaweza kuscore, Auba, Martinell na Pepe.
So Villar wana kocha mzuri kutuzidi.
Ila kwakua mimi siyo mzuri katika kusema makocha waondoke sina upande juu ya uwepo wa Arteta ni juu yake kuthibitisha kama anastahili kua pale ama la.
Arsenal kuikosa michuano ya Ulaya kwa mara ya kwanza ndani ya karne inatakiwa matokeo yake yaakisi uwepo wa kocha na uwepo wa mmiliki rafiki yake
Relief Mirzska