Mustafi amezikataa klabu tatu zilizomfuata. Anataka aende Barcelona au Milan tu.
Inatarajiwa Ozil mpaka J3 awe kasaini na Fenerbahce. Ila anaweza akaenda USA pia. Sokratis naye safari inanukia.
Fabrizio Romano anasema Arsenal wameanza mazungumzo na Draxler, Buendia na Aouar. Katika hao 3 kipaumbele cha Arsenal ni Aouar. Na kwa maelezo yake anasema Arsenal ilikua inataka kuwatoa Ozil na Sokratis ili kuweza kufund usajili wa CAM yeyote kati ya hawa 3.
Ilitarajiwa awe Brandt ila klabu yake midfielder tegemeo kaumia hivyo hawawezi mtoa Brandt.
Sa katika hizo options 3 zilizopo tutegemee nini?
Tuanze na Draxler; jamaa yuko vizuri, anajua kudribble, pasi, ana skills, anajua ni muda gani timu inahitaji kukomaa ili kupata goli na ana fighting spirit kama tunavyojua wajerumani walivyo.
Lakini jamaa ana kiburi, akiwa Wolfsburg akawa anafosi kuondoka kwenda Bayern mtiti na moto aliouwasha pale ilikua si mchezo. Wolfsburg ikajikuta inapambana isishuke daraja huku ina kiungo anayegawa dressing room. It was a disaster. Akiwa PSG wakiwa wanacheza na Madrid baada ya first leg kupigwa 3 - 1 Emery akamuinua Draxler ili aingie Draxler akiwa anajiandaa kuingia PsG ikapata goli na kua 1 - 1.
Emery akamrudisha Draxler bench, akaja kumuingiza zikiwa zimebaki dakika 6.
Baada ya mechi Draxler aliwaka sana. Akisema haelewi ni vipi kocha hakumuingiza muda ule ule kisa ubao kusoma 1 1 wakati haiwasaidii wao psg. Alilambwa benchi na Emery baada ya pale.
Narudi