Stats zinasema Mari alitoka njia yake na kwenda kupiga a shot on target juzi dhidi ya Brighton. Beki mwingine ambaye anaweza kucheza 1 2 na mkaenda kufunga na au akafunga ni Sergio Ramos wa Madrid.
Nilivyoona alichofanya Mari nikajiuliza kama yupo njiane kuelekea kua completed player. Tukiulizwa completed player tutamtaja messi na ronaldo na tutasema jinsi wanascore, clinical finishing na skills za kudribble n.k ila hiyo inawafanya wawe completed forwad na completed striker respectively.
Completed player ni kama Ramos, anakukaba akiambiwa akabe, anakufunga akitakiwa kukufunga. Historically tuna Gentle Giant, kuna mechi alikua anachezeshwa beki na zingine anawekwa forward na anaperform kwa kiwango kilekile.
Kwa sasa haina kupinga kwamba Bukayo Saka ni completed player, amecheza kama beki wa kushoto kwa kiwango, amecheza kama winger wa kushoto kwa kiwango, amecheza kiungo kwa kiwango na sasa anacheza kama winger wa kulia. Na anaperform vilevile.
Ile shot ya Mari imefanya nijiulize kama Mari ndipo anapoelekea, kama ni ndiyo, then yupo kwenye klabu salama na Arsenal ipo kwa mchezaji salama.