Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Mimi ningekuwa Emery ningehakikisha Calum Chambers anarudi kucheza kwenye position yake hapo nyuma kati then Bellerin aanze beki ya kulia... Kiukweli siku Back four ikiwa na Xhambers, Holding, Tieney na Bellerin halafu namba sita Torreila,tutarudisha heshima yetu iliyoanza kupotea!.. Tatizo kocha wetu mkuda sana, haeleweki kabisa!..
Haiwezi tokea kwa huyu muhindi mi nlishasema ikitokea ntamsupport ije mvua ije jua
 
Umeongea fact tupu

Kweli aweke hawa vijana ,kati anaweka LT11 KATIKA mfumo wa 4-1-3-2 then mbele ya lt11 anawaweka Mateo- Ozil-ceballos mbele Pepe na Auba au Laca na Auba

Mmoja anaanzia benchi


Au apange hivi

Leno.

Bellerin. Holding. Chambers. Tierney.

Torreira.
Guendouzi. Ceballos/Ozil.

Pépé. Lacazette. Auba.

That’s the team I want week in week out for the rest of this season


View attachment 1237137
Yaani we unachokiwaza ndo kabisa hakiwezekani labda apangiwe kikosi ,kweli Xhaka akae bench eti Lt11 na Ozil waanze kwa X1 ya Emery 😂😂😂. Wachezaji wapo wazuri ila anafanya watu wawaze kusajili kila siku.
 
- OFFICIAL
#Arsenal Game at Boxing day against Bournemouth will take place on Thursday, December 26th (3pm)

Arsenal will face #Chelsea and #ManchesterUnited teams at the emirates stadium in 48 hours.

Chelsea on 29 December 2 GMT AND THEN MANCHESTER ON 1 January 8 GMT. )
Hawa nao wanatupangia game kama hizi kibwegebwege tu ili tudrop point kwa wachovu hao.
 
Yaani we unachokiwaza ndo kabisa hakiwezekani labda apangiwe kikosi ,kweli Xhaka akae bench eti Lt11 na Ozil waanze kwa X1 ya Emery . Wachezaji wapo wazuri ila anafanya watu wawaze kusajili kila siku.
Najua yule muhind hawez kupanga kikosi kizuri hata siku moja

Hadi atafukuzwa hata kuja kupanga kikosi kizuri hata siku moja

Combo ya Xhaka/mateo-lt11-ceballos

Haji kuipanga had anaondoka Arsenal , anaweza kuja kuipanga muda umeshaenda
 
Mourinho says he doesn't keep runner-up medals so he threw it to an Arsenal supporter. #CFC

2nd August 2015
 
KUMPIGIA KURA MATEO GUNDUZ KWENYE TUZO ZA GOLDEN BOY FATA LINK HAPA

#GoldenBoy,

Golden Boy 2019: ecco i 20 finalisti. Vota e partecipa al sondaggio! Tuttosport on Twitter

BOFYA ,UTAKUTA MAJINA MENGI TAFUTA LA MATEO ,KISHA BOFYA ,THEN NENDA CHINI UTAKUTA SEHEMU YA KO VOTE ,BOFYA

Utakuwa umemaliza
Top 4 leading golden young boys
1:Mateo guendouz 10% 1800+ votes
2:mason mount 10% 1700+ votes
3;jodan Sancho 8% 1289
4;joao Felix 8% 1215
 
Aubameyang could score his 50th goal before reaching his 80th appearance for Arsenal. Including 14 assists... That’s one of the best records I’ve seen from any player in the Prem
IMG_20191019_071013.jpeg
 
Kurejea Kwa Lacazette Mpambanaji Wa Nyakati Ngumu

Binafsi Mpaka Sasa Nathubutu Kusema Yule Lacazette wa Olimpique Lyon Bado Sijamuona Rasmi Pale Emirates Tangu Atue Pale Msimu wa Mwaka Juzi Lakin Bado Haijazuia Yeye kuwa Mmojawapo wa Wachezaji Wetu Bora

Hakuna Asiyetambua Msimu Uliopita Huyu Ndo Mchezaji Wetu Bora Wa Msimu Mbele ya Wote Waliokuwemo na Kitu Kizuri ni Kwamba Kachaguliwa na Sisi Wenyewe Wenye Team yaani Mshabiki na Wachezaji Wenzake..

Lacca kidogo Majukumu yake Pale Kwetu ni Tofauti na Akipotoka Haswa katika Hii Emery Era Amekuwa akitumika Kama Ngazi au Anatumika Kama Sehemu ya Team Ya Kufanya Auba Afunge Magoli Kwa Wepesi yaani Huyu Jamaa Pale Kwetu Amekuwa kama Msaidizi wa Auba Au Ngazi ya Auba Kwenda Kuonana na Makipa ..Auba Anaweza Tokea Kushoto ila Majukumu yake Yanabakia Yale yale Ya Kuingia Nyavuni

Lacca anatoa Vitu Vingi Tofauti na Kufunga Ndio Maana Mda Mwingi Anautumia Nje ya Eneo ambalo Linamfanya Asiwe na Magoli Mengi Ingawa anahitajika Pia Kufunga

Linapokuja Suala la Wapinzani Wagumu au Wanaotulemea Tumekuwa Tunamtumia Sana Kukaa nao na Kuhakikisha Kule Mbele Mabeki Hawapumui na Zaidi Amekuwa akitupatia Magoli Muhimu Kwenye Zile Big Moment

Binafsi Natamani Sana Lacca afunge Sana Kuonyesha Ubora wake Aliokuwa Nao Kipindi Yupo Lyon ila Shida Ubora Wao wote Upo Katikati yan Striker Ye na Auba Kwaiyo Lazma Watanyang’anyana

Muhimu ni Team Kwanza na sio Ufungaji Bora Ama Uchezaji Bora kwaio Huyu Jamaa Akitupatia Hata Goli 15 za Kiume yan Zile Goli Unakaa Kwenye Mechi Haujui Linakuja Saa Ngap na Linatoka Wap Halafu Anafunga Hapo ndo Huo Huitwa Uanaume wa Mechi za Kiume

Nategemea Makubwa Sana Kwao na Auba Haswa Ukizingatia Msimu Huu Auba Kajiongeza Anaweza Kusogea nao Kukaa nao Tofauti na Mwaka Jana pia Msimu Huu Auba Hakosi Magoli Kama Mwaka Jana ...

LACA mwenyewe ameshasema EPL bado haijamshuhudia lacazette bora kabisa

Hatutegemei Kuchukua Kombe la ligi Wala Kumaliza Juu ya City na Liverpool lakin Top Four Kwetu ni Lazma na Pia Tunataka Tutumie Vizur Mwanya wa Wenzetu Walioanza Vibaya

Ila Unai Hatabiriki Aisee..
IMG_20191011_170714.jpeg
 
OZIL master wa Assist

Binafsi silaumu kwa mchezaji wa kariba ya Ozil kuwekwa bench...
Kuna kipindi sikuwa namuelewa kabisa huyu mchezaji. Hata kipindi wakati Sanchez anataka kuondoka kuna mtu alishawahi kuniuliza 'hivi kati ya Sanchez na Ozil ukiambiwa uchague mmoja aondoke utamchagua nani?'
Kwa haraka nilijibu Ozil lakin baada ya kutafakari nijicheka sana.

Ozil ni mtu wa kipekee sana, kuna kitu tunakikosa kwenye timu yetu kwa sasa. Hatuna mtu wa kupiga risk passes.

Hii namaanisha mtu wa kupiga pass ambazo kama zikipita mabeki basi hatari yake ya kusabisha goli ni zaid ya 90%.

Viungo wetu wengi tulionao ni wale ambao wakifika eneo la mita 30 kutoka lango la mpinzani basi atapiga pass kwa mtu ambae yuko karibu na ana uhakika pass itafika bila kupotea ( square pass).. yani namaanisha kwa mtu ambae watu wengi wanaona kuwa lazima atapewa pass tu mchezaji yule..

Hii inarahisisha hata kwa mabeki kumkaba mtu kirahisi na kumnyima nafasi kwakuwa walishajua atapewa pass na kweli anapewa.

Sasa hii inakuwa tofauti kwa upande wa Ozil.
Yeye akifika eneo la kuanzia mita 30 kutoka lango la mpinzani huwa anakua na jicho la tofauti kabisa, anapiga pass ambayo kama ikipita lazima isababishe madhara hata kama haitakua goli basi lazima Auba ama Laca atakosa goli litakalokuacha mdomo wazi..
Anapiga pasi kwa mtu ambae hujamdhani kabisa. Anaweza akageuka kushoto(kwa Kolasinac) afu akajikunja kama samaki kupiga pass kulia(kwa Belle)
Hata kama haitakua ni pass ya mwisho (assist) basi itakuwa ni pass inayomrahisishia mtoa assist apige pasi yake ki rahisi zaidi.
Na kwa Ozil hizi pass uwezo wake wa kuzifikisha kwa mtu ni zaid ya 50% .
Wachezaji wa namna hii ni wachache sana, unaweza kumpata labda Cazorla, Wilshire,David Silva, Fabregas Debruyne nk.

Tukubali tukatae, ukimtoa Ozil mtu wa kuvaa viatu vya kutimiza hili jukumu kwa sasa hatuna kwenye kikosi chetu, na waliopo hata wakijaribu ni mara chache sana wameweza kusifikisha hizi pass maeneo husika....
Akicheza mtu kama Ozil utaona hata kama hatufungi magoli mengi lkn unaona kuna kosakosa nyingi sana za magoli ya wazi..
Lkn kwa wachezaji tulionao nafasi za magoli na hata kosakosa huwa ni chache sana

Kwaio binafsi sipingi Ozil kukaa bench lakin je, ni nani wa kuvaa viatu vyake na akatengeneza muunganiko na kazi rahisi kati ya kiungo wakabaji na striking force yetu??
IMG_20191015_194201.jpeg
 
Tumpigie huyu mtoto iwe tunamkubal au hatumkubali, kama Chelsea wanampigia MTU ambaye msimu uliopita alikuwa championship ,sisi ni nan tu muache Mateo

Pigen kura.....
Muwape judges kaz .....thou kura hazimpi MTU ushindi ila n kigezo kinachomsogeza kwenye ushindi


mpigieni Matteo gundouz kura awe golden boy

KUMPIGIA KURA MATEO GUNDUZ KWENYE TUZO ZA GOLDEN BOY FATA LINK HAPA

#GoldenBoy,

Golden Boy 2019: ecco i 20 finalisti. Vota e partecipa al sondaggio! Tuttosport on Twitter

BOFYA ,UTAKUTA MAJINA MENGI TAFUTA LA MATEO ,KISHA BOFYA ,THEN NENDA CHINI UTAKUTA SEHEMU YA KO VOTE ,BOFYA
 
Mimi ningekuwa Emery ningehakikisha Calum Chambers anarudi kucheza kwenye position yake hapo nyuma kati then Bellerin aanze beki ya kulia... Kiukweli siku Back four ikiwa na Xhambers, Holding, Tieney na Bellerin halafu namba sita Torreila,tutarudisha heshima yetu iliyoanza kupotea!.. Tatizo kocha wetu mkuda sana, haeleweki kabisa!..
hehehe
 
Arsenal will wear their ‘Bruised Banana’ away shirt when they play Sheffield United on Monday. #afc
IMG_20191019_121838.jpeg
 
Tumpigie huyu mtoto iwe tunamkubal au hatumkubali, kama Chelsea wanampigia MTU ambaye msimu uliopita alikuwa championship ,sisi ni nan tu muache Mateo

Pigen kura.....
Muwape judges kaz .....thou kura hazimpi MTU ushindi ila n kigezo kinachomsogeza kwenye ushindi


mpigieni Matteo gundouz kura awe golden boy

KUMPIGIA KURA MATEO GUNDUZ KWENYE TUZO ZA GOLDEN BOY FATA LINK HAPA

#GoldenBoy,

Golden Boy 2019: ecco i 20 finalisti. Vota e partecipa al sondaggio! Tuttosport on Twitter

BOFYA ,UTAKUTA MAJINA MENGI TAFUTA LA MATEO ,KISHA BOFYA ,THEN NENDA CHINI UTAKUTA SEHEMU YA KO VOTE ,BOFYA
Tayari nimempa dogo kura
 
Arsenal will have the chance to sign RB Leipzig's Dayot Upamecano next summer for £53m.

Leipzig are ready to accept a lower fee to stop the risk of losing him on a free when his contract expires in 2021,

[Kicker]
IMG_20191017_193356.jpeg
 
Lait ingekua arsenal na big match kila mtu angekua anasubir kikosi kitakuaje.

Ila Liverpool hapa unajua full mkoko bila kupepesa macho hawa ndio Kariba ya makocha ambao wanatafuta ushindi na makombe.
 
Back
Top Bottom