Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

tupo na mgonjwa wetu mara anapata nafuu mara anazidiwa sijui ugonjwa gani huu.

Yani mnakuwa aste aste kila gemu, presha juu mara chini..haya tusubirieni wanaume-Man city! mana mechi za leo wamecheza wavulana,ha ha...no offence,lol
 
watoto wamejua kukaba na wamejua kushambulia,sisi tumelala tu tunalzimisha pasi za kwenye box kila siku .au wachezaji wetu wana kalili sana kama mfumo wa elimu wa tanzania? mtu unashindwaje kusoma game?
 
Yani mnakuwa aste aste kila gemu, presha juu mara chini..haya tusubirieni wanaume-Man city! mana mechi za leo wamecheza wavulana,ha ha...no offence,lol
man city au unamaanisha man united lol? wewe nawe ukiona wakubwa wameteleza kidogo unaanza kuchanganyikiwa kwa furaha.

sisi tunalipa deni la uwanja hayo mengine yote bonus tu.tukimaliza kulipia uwanja tunakuja kuchukua makombe tena sasa kujaza makabati ya emirates.
 
Hehehe akina drogba mkiwazuia wasifunge mpaka dakika ya 60 basi game yenu. Ila wiki ijayo patamu kweli kweli.

yule squash na mwenzake wana nguvu ya kumkaba drogba? labda song acheze beki tano kidogo mvua inaweza kuwa ya rasha rasha.
 
Mkubwa are you serious?

Arsenal 2 West Brom 3 ,tena nyumbani
Tatizo letu ni viungo, nilishangaa Wenger aliamua kuanza na 4-4-2 halafu eti Diaby, Eboue na Song wote wameanza? huwezi kuanza na Diaby na Eboue kama unataka ushindi, aliwadharau West Brom, Diaby, Eboue na Song wanapoteza pasi hovyo na hawakawii kupigisha free-kick, ni too risky kuwaweka kwenye same line-up.
Sagna nae alikuwa bomu, Huyu Almunia tumeshamzowea, ingawa aliokoa penalti amefungwa magoli ya kizembe, yote haya ni Wenger dunia nzima ilimwambia asajili kipa na muda alikuwa nao tosha, hela alikuwa nayo, Wenger amelosti plot kiaina.
 
man city au unamaanisha man united lol? wewe nawe ukiona wakubwa wameteleza kidogo unaanza kuchanganyikiwa kwa furaha.

sisi tunalipa deni la uwanja hayo mengine yote bonus tu.tukimaliza kulipia uwanja tunakuja kuchukua makombe tena sasa kujaza makabati ya emirates.

Thanks mkuu, keyboard leo ina-type Man City tu..he he, muhimu kushabikia mana man utd wakifungwa jukwaa lake linajaa wapinzani na maneno ya kila namna..Phew, naombea ushidi wetu mana vinginevyo, itageuka huzuni..
Kumbe nyie shida kukamilisha deni tu?! basi kama ndo hivyo ilimradi uwanja ujae kupata mapato makubwa!
 
wewe na balatanda huwa nina waheshimu sana michango yenu! ligi ndo kwanza mechi ya sita! I hate wacha1 boflo ni mjinga sorry for being harsh

Why be sorry nafsi yako inakusuta? Ukweli siku zote unauma.

Khe khe khe kheeeeeeeeee na Jumapili tunawafunga Stamford Bridge mwaka huu mtaendeleza matanga tu. Ile Fweza mliyompa Almunia ndiyo ilikuwa ya mwisho sijui mtapata wapi mpunga wa kuwahonga mareferee. Tena uzuri leo katuonyesha sura yake khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeee.

Thanks mkuu, keyboard leo ina-type Man City tu..he he, muhimu kushabikia mana man utd wakifungwa jukwaa lake linajaa wapinzani na maneno ya kila namna..Phew, naombea ushidi wetu mana vinginevyo, itageuka huzuni..
Kumbe nyie shida kukamilisha deni tu?! basi kama ndo hivyo ilimradi uwanja ujae kupata mapato makubwa!
deni tu ndio tatizo letu ndio maana product zote tunajaribu kutengeneza wenyewe sio kama abromavich na yule sheikh mansoor na tajiri wenu lol.

tuna mchumi wenger timu inaendeshwa kibiashara kwa ajili ya faida sio kama chelsea kwa ajili ya kufuruhaisha mashabiki huku siku ya mwisho hasara tu.
anyway kesho wewe una haki ya kushinda manake wakubwa wote leo tumechemsha.
 
sasa kama odemwinge anatesa hivi drogba itakuwaje?
Mkuu Odemwinge ni quality kushinda Drogba, Drogba ni box man na an nguvu ila ameanza kukaa kwenye namba sio ya 30, kwa upande wa Ode yeye ni sawa na Anelka, anaweza kucheza right. left ama lone striker, japo sio jibaba lakini ana nguvu, anafunga mguu wa kulia, kushoto hata kwa kichwa, na anatumia akili sana, pia ana uwezo mkubwa wa kuzuia mpira wanaposhambulia.
 
mkuu mie namuheshimu drogba tuache ushabiki.
 
Hata mimi namheshimu na najua anatupa shida sana ila nilikuwa najaribu kusema huyu Ode nae ni quality na alistahili attention kubwa sawa na Drogba, huyu jamaa atang'ara sana na kama akiepuka majeruhi namtegemea katika top 4 ya wafungaji bora
 
Kumbe Chelsick wanafahamu wapinzani wao ni nani. Walikuwa wamelowa kama kuku aliyenyeshewa na mvua lakini baada ya mechi ya Emirates naona wamefufuka. Sasa kukata mzizi wa fitna mambo yote Darajani Jamapili ... .... ..... ongezeni bei ya sangwejes tu maana hamna fweza ... ... sisi tutalipa tu ili kuwaokoa na ukata.
 
Hata mimi namheshimu na najua anatupa shida sana ila nilikuwa najaribu kusema huyu Ode nae ni quality na alistahili attention kubwa sawa na Drogba, huyu jamaa atang'ara sana na kama akiepuka majeruhi namtegemea katika top 4 ya wafungaji bora

sawa sawa mkuu.

wachezaji wetu wanatuangusha sana.
 
sawa sawa mkuu.

wachezaji wetu wanatuangusha sana.
Ni sawa kabisa, yaani mechi ya leo walicheza kibishoo kabisa hakuna passion wako slow, hakuna movement wala penetration yaani ile staili ya Arsenal ilikuwa hakuna, wamekuja kuamka baada ya bao la 3 zikiwa zimebaki dakika 15, too late!! kwa kweli tunam-misi sana Fabregas, bila yeye hakuna uongozi kwenye pitch na zile killer penetration pass zinakosekana, inabidi dogo Wilshere ajitahidi sana kumsoma Fabregas wakati bado yupo nasi, nakumbuka baada ya mechi ya Blackpool Fabregas alipohojiwa na kuulizwa kwa nini alionekana kukasirika alijibu baadhi ya wachezaji dakika za mwishoni mwishoni walionekana kupoteza concentration yao na alisistiza ingawa tunaongoza mabao 6 inahitajika umakini mpaka filimbi ya mwisho,na vitu vidogovidogo kama hivi ndio vinatufanya kukosa ushindi, leo tulikuwa too sloppy, concentration ziro kabisa.
 
BTW ni vizuri wachezaji wajue hakuna lelemama, itawapa mwamko zaidi kwa mechi ya jumapili na mimi nangojea ushindi tu lazima tuwakung'ute Chelsick na kuwachekecha.
 
Back
Top Bottom