Arsenal ina wakati mgumu sana kupata manager ambaye atatuvusha katika dimbwi la kuwa mediocre team kwa miaka mingi, Wenger alikuja na kufanya kile alichoweza, kipindi cha Wenger tumepitia mengi kama timu, tumeweka records nyingi lakini pia tumeweza kuchezea kwenye uwanja mkubwa zaidi hivyo mapato ya timu kuongezeka. Alichofanya Wenger ni kuimarisha timu kimapato Ila alishindwa kutengeneza timu ya kushinda makombe makubwa, tangu 2006 CL final hatujawahi kufika zile heights tena.
Binafsi naamini Arteta, Henry au Vieira ni daraja moja la makocha hasa katika uzoefu. Je, arsenal board wanaenda na uzoefu, wanataka cheap au consistency? Pundits wengi wanaamini arsenal wanaangalia consistency na umri wala sio proven manager. Uzoefu wa Arteta kwa miaka miwili hautoshi kuwa strong candidate kuongoza timu kubwa kama Arsenal, likewise Henry au Vieira.
Lakini je, Arsenal wanakubali kuwa na budget ya kuleta big spenders kama Ancelotti, Allegri au Enrique? Hao ni big spenders, na kwa mpira wa kisasa huwezi kukwepa "spending big", if you want to win big, you've got to spend big and wise, ndio maana RM na Barca hawashuki kimafanikio, they spend.
Sisi ni mashabiki, tunapiga vuvuzela hata ziwa Tanganyika halivuki lakini tunaitakia mema timu yetu. Tusijemaliza msimu tukiwa nafasi ya 16.