Arsenal (The Gunners) | Special Thread

INAELEKEA Arsenal na Chelsea zinaweza kuwa na makocha wapya kuanzia Juni mwaka huu kama ubuyu unaoendelea kuvuma Ulaya utakuwa na ukweli ndani yake.

Kocha wa zamani wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel ameripotiwa kuipiga chini ofa ya klabu ya Bayern Munich iliyokuwa inamtaka kwa udi na uvumba kwa ajili ya kuanza mazungumzo na Arsenal ambayo imeonyesha nia ya kumtaka.

Munich ilikuwa inamtaka kocha huyo Mjerumani kwa ajili ya kuwa mrithi wa kocha wake wa sasa, Jupp Heynckes lakini ofa zake zote zimekataliwa kwa kile kilichoelezwa Tuchel anataka kwenda kufundisha nje ya Ujerumani.

Huu unaweza kuwa mwanzo wa mwisho kwa kocha wa muda mrefu wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye amekuwa klabuni hapo tangu mwaka 1996 na gazeti maarufu la michezo la Ujerumani Bild limedai kocha huyo tayari yupo katika mazungumzo na Arsenal kwa ajili ya kuchukua kazi ya Wenger.

Vilevile inadaiwa hata Chelsea inavutika na mpango wa kumchukua kocha huyo mwenye umri wa miaka 44. Chelsea inatazamiwa kuachana na kocha wake, Antonio Conte mwishoni mwa msimu lakini inaonekana Arsenal ndio imekaribia zaidi kumnasa Tuchel.

Tuchel amekuwa hana kazi tangu Mei mwaka jana baada ya kuachana na Dortmund siku chache baada ya kuipa Kombe la Ujerumani na anajulikana vizuri kwa bosi mpya wa masuala ya utendaji wa timu ya Arsenal, Sven Mislintat aliyechukuliwa kutoka Dortmund.

Wawili hao walifanya kazi pamoja Dortmund, ingawa hawakuwa na uhusiano mzuri sana. Hata hivyo, kwa sasa wanaweza kufanya kazi tena pamoja wakati huu Mislintat akitazamiwa kukisuka upya kikosi cha Arsenal.

Wakati Wenger akiwa amekalia kuti kavu, Chelsea pia kunaweza kuwa na mabadiliko baada ya wawakilishi wa kocha wao, Antonio Conte kufanya mazungumzo na klabu ya PSG ambayo inatazamiwa kuachana na kocha wake, Unai Emery mwishoni mwa msimu.

Matajiri wa PSG hawatazamiwi kuongeza mkataba wa kocha huyo ambao unatazamiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu kutokana na kushindwa kuonyesha makali yake katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya ambapo PSG ilitupwa nje na Real Madrid.

Na wakati huohuo Chelsea nayo haitazamiwi kubaki na Conte ambaye amekuwa na msimu mbovu mpaka sasa ikishika nafasi ya tano katika msimamo wa LIgi Kuu ya England licha ya kutwaa ubingwa msimu uliopita.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Guardian la Uingereza, PSG imemfuata Conte na kuanza maongezi naye huku kukiwa na maendeleo makubwa katika dili hilo ambapo Conte, 48, atakuwa na ongezeko la Pauni 500,000 katika mshahara wake wa sasa.

PSG ina machaguo mengine mbalimbali klabuni hapo ikiwemo Jose Mourinho, Mauricio Pochettino, Diego Simeone na Max Allegri lakini Conte anaonekana kuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kupatikana kuliko makocha wenzake.

Inadaiwa Conte anajisikia kuanza upya kwingine huku akiwa anavutiwa na mpango wa PSG kutumia pesa nyingi katika dirisha kubwa linalokuja kwa ajili ya kukisuka kikosi hicho ambacho kimekuwa na nia kubwa ya kutwaa ubingwa wa Ulaya.

Conte amekerwa na jinsi ambavyo msimu wa Chelsea ulivyoenda ikiwa imebakia katika michuano ya FA tu huku ikiwa imetupwa katika michuano mbalimbali ikiwemo Ligi ya Mabingwa Ulaya na haina matumaini ya kutetea taji lake.

Kocha huyo pia amekuwa katika mapambano ya mara kwa mara katika vyumba vya kubadilishia nguo Stamford Bridge na inadaiwa baadhi ya wachezaji mastaa klabuni hapo hawatafurahia kama atakuwepo tena msimu ujao.

BAYERN Munich ina majanga, straika wake Robert Lewandowski amegoma kusaini akiitaka Real Madrid, huku kocha iliyekuwa ikimpigia hesabu kali, Thomas Tuchel kapiga chini ofa za klabu hiyo.

Lewandowski mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu lakini Tuchel, Kocha wa zamani Borussia Dortmund anawindwa kwa kiasi kuikubwa na vinara hao wa Bundesliga kuchukua nafasi ya Jupp Heynckes mwisho wa msimu. Heynckes, alirudishwa klabuni baada ya kutimuliwa kwa Carlo Ancelotti, mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu na Bayern italazimika sasa kusaka kwingine baada ya Tuchel kuwachomolea.

Tuchel alichukua nafasi ya Jurgen Klopp kikosini Borussia Dortmund na kutengeneza timu moja matata Ulaya kabla ya kunyakuliwa na Liverpool.

Kocha huyo anatakiwa na Chelsea na Arsena baada ya makocha wao kuonekana kuzingua.

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte anatajwa kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu Stamford Bridge baada ya kuvurugana na mabosi wa klabu huku Arsene Wenger, mkataba wake umesalia miezi 12 na utasitishwa endapo Arsenal na utaangaliwa endapo itatwaa ubingwa wa Europa na kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Tuchel ndiye aliyewapika wachezaji waliotua Arsenal dirisha la Januari, Pierre-Emerick Aubameyang na Henrikh Mkhitaryan walipokuwa Dortmund.

Habari zilizopatikana baadaye jana zilisema kuwa kocha huyo ameshatua Emirates na kilichobakia ni suala la muda tu, Wenger akusanye virago vyake ili achukue ukanda.
 
Tetesi

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema anataka sana kiungo wa kati Jack Wilshere asalie katika klabu hiyoo. Mchezaji huyo wa England wa miaka 26 amekuwa kwenye mvutano na klabu hiyo kuhusu mkataba baada yake kuombwa akubali kupunguziwa mshahara. (Star)

Mkufunzi wa zamani wa Borussia Dortmund Thomas Tuchel angependa zaidi kwenda Bayern Munich kurejelea kazi ya ukufunzi na si kwenda Arsenal, kama zilivyokuwa zimedokeza tetesi kwamba atakwenda kumrithi Wenger. (Sky Sports)
 
Back
Top Bottom