Cheki hapa ratiba iliyobaki kwa timu ya arsenal na wanavyotabiriwa namna watakavyomaliza msimu kwa pointi watakazovuna.
ARSENAL
Msimamo: Nafasi ya Sita
Pointi: 48
Mechi: 30
Ratiba mechi zilizobaki
Arsenal v Stoke City
Arsenal v Southampton
Newcastle v Arsenal
Arsenal v West Ham
Man United v Arsenal
Arsenal v Burnley
Huddersfield v Arsenal
Arsenal inasubiri muujiza tu ndiyo utakaowafanya wamalize Ligi Kuu England msimu huu wakiwa ndani ya Top Four katika msimamo. Kwa sasa wamekusanya pointi 48 tu katika mechi 30 walizocheza. Kuifikia timu inayoshika nafasi ya nne kwa sasa, inahitaji kushinda mechi tano, huku wenzao hao walipo kwenye nafasi hiyo ya nne, Tottenham wasiwe wameshinda mechi yoyote wala kutoka sare. Arsenal imebakiza mechi nane kumaliza msimu na kama watashinda zote basi wataweza kumaliza msimu wakiwa na pointi 72, ambazo haziwafikii kabisa wenzao waliopo juu kama utabiri utakwenda kama ulivyotabiriwa kwamba Man United itamaliza ligi na pointi 82, Tottenham pointi 77, Liverpool pointi 76 na Chelsea pointi 76. Kwa maana hiyo, Arsenal hawataweza kumaliza Ligi Kuu England msimu huu ndani ya Top Four.