Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Kweli wewe ni nzi. Tunaposema kipaji cha mchezaji kimekuzwa we mean kajulikana akiwa wapi na kakuzwaje..

Is that it? Don’t give up so easily bruv!

Sasa Ajax na Arsenal ni level moja.

Ni swali ama? Kama ni swali, jibu ni obvious, Ajax wapo wayyyy above Goons! They have won UCL 4 times, Europa Cup 1 time, and Intercontinental cup twice.

They are have the best youth system in the world, having produced: Kluivert, Bergkamp, Sneijder, Van Basten, Cruyff, van der Sar, van der Vaart, de Boer brothers, Edgar Davis etc.

Sasa Goons mna nini cha kujivunia above Ajax FC kweli?
 
Is that it? Don’t give up so easily bruv!



Ni swali ama? Kama ni swali, jibu ni obvious, Ajax wapo wayyyy above Goons! They have won UCL 4 times, Europa Cup 1 time, and Intercontinental cup twice.

They are have the best youth system in the world, having produced: Kluivert, Bergkamp, Sneijder, Van Basten, Cruyff, van der Sar, van der Vaart, de Boer brothers, Edgar Davis etc.

Sasa Goons mna nini cha kujivunia above Ajax FC kweli?
Kumbe kuna watu na viatu humu ndani
Has your brain choose this post you posted the best among all the points that your brain has?
Nottingham forest has 2 UCL cups while PSG has no UCL cup so NG>PSG isn't it
Ac Milan has more European cups than Barcelona.Is it true that ac Milan is greater than barca?
Scratch your big head
 
Lacazette ataikosa game ijayo dhidi ya Utd amepata majeraha (groin) kwenye game ya jana dhidi ya Huddersfield.
c32eb81ee7a9396226ea7d0e1cb274b9.jpg
 
Tetesi

ARSENAL KUMSAJILI FEKIR


Arsenal itafanya mpango wa kumsajili Nabil Fekir kutoka Lyon, kwa mujibu wa TuttoMercatoWeb .
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 24 sasa amekuwa akifuatiliwa na Barcelona, Juventus na Atletico Madrid, lakini Gunners wanatumai kumsajili kuwa mshambuliaji wao.
 
Tetesi

ARSENAL WANAPEWA NAFASI KUBWA KUMSAJILI JANKTO


Arsenal wanapewa nafasi kubwa kumsajili Jakub Jankto kutoka Udinese baada ya Juventus kuacha mpango wa kumsajili, kwa mujibu wa Calciomercato .
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa akifuatiliwa na klabu zote mbili, lakini miamba wa Serie A hawapo kutoa fedha nyingi kumsajili hivyo kuwaachia Gunners nafasi.
 
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anahofia mshambuliaji Alexandre Lacazette ''hatakuwa uwanjani kwa muda'' baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu siku ya Jumatano, katika mecho ambayo walipata ushindi wa magoli 5-0 dhidi ya Huddersfield.
Lacazette, 26, alifunga bao la kwanza lakini alitolewa uwanjani wakati wa mapumziko na nafasi yake kuchukuliwa na Oliver Giroud.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amefunga magoli saba kwa Gunners tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka Lyon mwezi Julai kwa kitita cha £46.5m.
''Ni bayana hatashiriki mechi ya wikendi hii,'' Wenger amesema.
''Alipata jeraha kwenye kifundo cha mguu wake. Atakuwa nje ya mchezo kwa muda.'
 
Arsenal ilisubiri kwa hamu kumwona Santi Cazorla akirejea dimbani kusakata kabumbu, lakini kwa bahati mbaya anafanyiwa upasuaji tena
Santi Cazorla amebainisha kuwa pamoja na kusubiriwa kwa muda mrefu kurejea kazini Arsenal, majeraha mapya yataendelea kumsubirisha zaidi.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye hajagusa mpira tangu Oktoba 2016 kutokana na maheraha, alitarajiwa kurejea kibaruani Mwaka Mpya.
Akiwa ameshafanyiwa upasuaji mara nane mwaka jana, ikiwa ni pamoja na mchakato tata wa kuhamisha ngozi kutoka mkononi mwake na kuipachika kwenye kifundo cha mguu wa kushoto, Cazorla atapigwa kisu tena kurekebisha tatizo jipya.
"Kutokana na matatizo ya kwenye tendoni ambayo ilijeruhiwa, nalazimika kurejea kwenye chumba cha upasuaji kwa mara nyingine tena," alituma chapisho kwenye akaunti yake binafsi ya Twitter.
"Naendelea tena kusubiri kurejea dimbani, lakini bado nina imani na mwamko kuwa nitarudi katika ubora wangu kucheza mchezo ninaoupenda, Soka."
Bosi wa Arsenal ameelezea jeraha la Cazorla la muda mrefu kuwa "baya zaidi" alilowahi kuona kwa kipindi cha miongo mitano alichodumu kwenye soka.
 
740e6eefccb9b74747c53624b83aca12.jpg

Hii ni banner yenye ukubwa wa 20 ft kesho itatumika wakati wa game na wimbo wa Ozil utaimbwa na mashabiki,naona tumeshindwa kumpa sarafu tumeamua kumtongoza kwa maneno tu.
 
Mbadala wa Ozil na Sanchez kwa sasa siuoni. Kwao wako sahihi nadhani they are approaching 30yrs retirement kwenye football inakaribia. Ni wakati sahihi wa kutafuta high salary. Afterall they are good players...
 
Mbadala wa Ozil na Sanchez kwa sasa siuoni. Kwao wako sahihi nadhani they are approaching 30yrs retirement kwenye football inakaribia. Ni wakati sahihi wa kutafuta high salary. Afterall they are good players...

Kwa hali ya soka la sasa wako sahihi sana ku-demand mshahara mkubwa na sina tatizo kabisa na uamuzi wao wa kuondoka naona Arsenal haitaki kabisa kubadilika kwenye hili la maslahi.
 
Tetesi
ARSENAL NA MAN CITY ZAMWANIA EVANS


Beki wa kati wa West Brom Jonny Evans amezivutia Manchester City na Arsenal kwa ajili ya uhamisho wa Januari, kwa mujibu wa The Telegraph .
Ilitipotiwa kuwa ofa ya Arsenal ya £25 milioni ilikataliwa Agosti 31 kwa ajili ya mchezaji huyo, kwani WBA wanataka kiasi kisichopungua £30m.
 
duh sikuwahi kufikiria Ozil angesepa mapema ivi ila nilikua na uhakika Sanchez anapita tu,vunja kibubu kaka tumpe uyu muarabu sarafu anatusaidia sana.
Yes anatusaidia sana sawa
Ila pesa anayotaka ni karibia mara tatu na anayolipwa sasa
Kwanini tusisajili mastaa wa maana zaidi ya mmoja tukawalipa hiyo pesa sisi sio Paris
Man u wenyewe hawako tayari kumpa hiyo pesa Pogba ndo anaongoza man u analipwa 290000 ozil anataka 370000.
370k pounds? for what purpose?
KDB ndo mwenyewe pale city kama akipewa new contract utasikia mshiko wake unarange 200000-290000 sasa yeye ozil anataka 370k mtu mwenyewe mzuri timu ikiwa fomu ina attack
Tukizidiwa utatamani apigwe hata bench hakabi
Harafu anataka kulipwa zaidi ya Cristiano Ronaldo? Hapana nimekataa
 
Arsenal habari za timu vs Man United

Alexandre Lacazette alitolewa kwenye mechi ya Jumatano baada ya kupata majeraha.
Arsene Wenger alisema baada ya mechi kwamba "atakosekana dimbani kwa muda".
Olivier Giroud anaweza kuanza kufuatia kukosekana kwa Mfaransa mwenzake.
Alex Iwobi atakuwepo mzigoni baada ya kupona majeraha ya mguu wake.
Danny Welbeck yupo fiti kuikabili klabu yake ya zamani. Muingereza huyo amefunga mara tatu mfululizo dhidi ya waajiri wake wa zamani.
 
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa hatarajii kama Jose Mourinho atatumia mbinu za kujihami Man United watakaposafiri kwenda Emirates
Mashetani Wekundu wameshindwa kuifunga timu yoyote katika sita kuu kwenye mechi ya ugenini chini ya Mourinho katika matukio saba tangu achukue mikoba kuinoa timu hiyo mwaka jana, akiambulia sare tatu na kupoteza nne.
United pia wamefanikiwa kuweka kimiani goli moja katika mechi waliyofungwa 2-1 na Tottenham Hotspur miezi sita iliyopita - na walikosolwa hivi karibuni kwa mbinu walizotumia kwenye sare isiyo ya magoli dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Anfield.
Wenger anaamini kuwa wageni wake watajaribu kutafuta mbinu kuongeza mashambulizi na kukaba pia katika mechi yao ya Jumamosi jioni, hata hivyo, aliwaambia waandishi: "Sitarajii jambo jipya [kiulinzi]. Man United ni timu imara na natarajia tutaweza kuyakabili matatizo watakayotusababishia.
"Watashambulia pia. Hawatakaba tu. Ni mechi baina ya Arsenal na Man United nyumbani kwetu. Nahitaji tu kujidhatiti na kuandaa vema timu yangu, na kuipa timu yangu nafasi nzuri kushinda mechi hiyo. Man United wanafanya vizuri kwa sasa, tunafanya vizuri pia kwa sasa, kwa hiyo inaonekana itakuwa mechi yenye mvuto."
Wenger, ambaye atamkosa mchezaji wake ghali zaidi Alexandre Lacazette dhidi ya United, amefanikiwa kukipandisha kikosi chake nafasi ya nne kufuatia ushindi wa mechi tatu mfululizo.
 
Back
Top Bottom