Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Burnley ni miongoni mwa timu zinazosumbua sana kwa sasa kwenye ligi,,,wamempiga Chelsea,,,na wametoka sare na both Liverpool and Tottenham ambazo zote n timu kubwa so mashabiki sometimes tunapaswa kuangalia mpinzan tuliyecheza nae kwanza kabla ya kuanza kuilaumu timu
 
745752ef048b0f67241463201d4154b9.jpg
 
Alexis Sanchez amefunga penalti katika muda wa kuyoyoma na kuipa Arsenal ushindi dhidi ya Burnley uwanjani Turf Moor.
Ilikuwa ni marudio ya mechi ya msimu uliokwisha kati ya timu hizo mbili uwanjani Emirates wakati raia wa Chile - Sanchez alipofunga bao kunako dakika 98 kushinda mechi hiyo.
Ilikuwa pia ni mara ya tatu mtawalia kuwa Gunners imepata ushindi katika muda wa mwisho wa mechi dhidi ya Clarets.
Pointi tatu iliyojinyakulia Arsenal inaikweza timu hiyo hadi katika nafasi ya nne kwenye orodha wakati wakisubiria mechi yao dhidi ya wapinzani wao wa Londona kaskazini Tottenham, waliotoka sare ya 1-1 dhidi ya West Brom Jumamosi.
Matokeo hayo yalikuwa ni kipigo kwa upande wa Sean Dyche ikiwa wamefanikiwa ushindi wa mechi zao mpaka sasa ikiwa walionekana kama watanyakuwa japo pointi moja, kabla ya refa Lee Mason kuashiria sehemu ambapo mlinzi James Tarkowski alimsukuma Aaron Ramsey.
Petr Cech ndiyo aliyekuwa na kibarua kigumu kati ya makipa wawili , akifanikiwa kuokoa mikwaju miwili na kumnyima goli Johann Berg Gudmundsson.
Robbie Brady pia alikuwa na 'free-kick' kuelekea kona iliosukumwa kando na Cech.
 
Inafahamika kuwa ofa ya washika mtutu wa London ya £90m ilikataliwa na Monaco kwa ajili ya Mfaransa huyo katika dirisha la uhamisho wa majira ya joto, kadhalika Liverpool nao wanaaminika kuvutiwa na mchezaji huyo.
Kwa mujibu wa Daily Mail, miamba hao wa London Kaskazini watarejea tena Januari kwa ajili ya mchezaji huyo lakini hawatatoa ofa kubwa kama walivyofanya majira ya joto.
Ripoti zinadai kuwa Arsene Wenger ana shauku kubwa ya kuleta mchezaji mahiri katika safu ya mashambulizi kikosini mwake ikiwa Mesut Ozil na Alexis Sanchez wataondoka klabuni hapo mwakani.
Lemar, ambaye amejiunga na Monaco 2015 kutoka Caen, amecheza mechi 103 kwa miamba hao wa Ligue 1, akifunga magoli 20 na kutoa pasi 25 za goli.
 
ARSENAL ZINAMTAKA LIVERPOOL DRAXLER


Arsenal wameungana na Liverpool katika mbio za kuiwania saini ya Julian Draxler kutoka Paris Saint-Germain, kwa mujibu wa The Mirror .
Inafahamika kuwa Liverpool wanamhusudu mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani na wanataka kumsajli kwa mkopo, lakini PSG wapo tayari kumuuza.
 
Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa afisa mkuu mtendaji wa klabu hiyo Ivan Gazidis hausiki na mpango wa kuwanunua wachezaji kufuatia mabadiliko yaliofanyika katika klabu hiyo(Daily Mail)
 
Tetesi

Arsenal ni miongoni mwa vilabu kadhaa vya ligi ya Uingereza wanaotaka kumsajili Novara Calcio mwenye umri wa 20 raia wa Uholanzi Alessio da Cruz. (Daily Mirror)
 
Tetesi
Beki wa Arsenal na Ufaransa Laurent Koscielny, 32, anataka kumaliza mchezo wake katika klabu ya Lorient, kulingana na rais wa klabu hiyo ya Ufaransa (Canal+, via Goal)
 
Back
Top Bottom