Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

23168044_1499516240131962_4098236188226425992_n.jpg
 
Man city ikiwa kwenye kiwango kizuri ilimpiga Man Utd 6 lakin ikaishia kupigwa na arsenal. Leicester city walibeba ubingwa wakazicharaza timu zote uingerza lakini walipigwa ndani nje na arsenal na kipigo kimoja kwa Liverpool. Siibezi arsenal ni timu nzuri inahitaji marekebisho machache sana.
 
Arsenal imewatuma wasajili wake kumchunguza kinda wa Manchester United Bobby Duncan akicheezea timu ya Uingereza ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 17 wiki hii.Duncan ni binamu yake mchezaji wa zamani wa Liverpool Steven Gerrard. (Daily Mirror)
 
Beki wa kulia wa Arsenal Bellerin, 22, anasakwa na Juventus na tayari imebainika kwamba klabu hiyo imewasiliana na beki huyo wa Uhispania kupitia wawakilishi wake.. (Sun)
 
OZIL ANAITAKA JEZI YA WILSHER NA.10


Mesut Ozil anaitaka jezi namba 10 ya Jack Wilshere kama sehemu ya mkataba wake mpya katika klabu ya Arsenal, kwa mujibu wa The Sun .
 
OZIL ANAITAKA JEZI YA WILSHER NA.10


Mesut Ozil anaitaka jezi namba 10 ya Jack Wilshere kama sehemu ya mkataba wake mpya katika klabu ya Arsenal, kwa mujibu wa The Sun .
Aende tu nae asitutie presha..
 
TETESI
Arsenal wana mpango wa kumsajili Zaha ambae ni mshambuliaji wa Palace kwa kitita cha £ 35m kwenye kipindi cha dirisha dogo.
64ac48f05d3837b6fd0496aac9d3a6cf.jpg
 
Jmosi na fit again Harry Porter Kane?
Ehehehe nakupigia dim lights hapo ba hunipati tena!
See you tena May
 
Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 31, anasema hajutii kwa kusalia na Gunners na kutojiunga na Everton, West Ham au Marseille. (Sunday Telegraph)
 
Mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 31, anasisitiza kuwa atakuwepo kwenye klabu hiyo. (Independent)
 
Arsenal wanakaribia kukamilsha dili ya kumsajili mshambuliaji wa Lyon, Nabil Fekir kwa pauni milioni 60 ambaye kuwasili kwake kutafufua kuondoka kwa Mesut Ozil, 29 na Alexis Sanchez, 28.
 
Tetesi
ARSENAL YAKARIBIA KUMNASA FEKIR


Arsenal wanakaribia kumsajili mshambuliaji wa Lyon Nabil Fekir kwa kitita cha paundi milioni 60, kwa mujibu wa Daily Star .
 
Tetesi
ARSENAL YAACHA KUMFUKUZIA LEMAR


Arsenal wameamua kuachana na mpango wa kumsajili Thomas Lemar na wanaangalia mbadala mwingine kwa mujibu wa habari kutoka Mirror.
Ofa ya Gunners ya paundi milioni 90 ilitolewa nja na Monaco kwa ajili ya nyota huyo wa Ligue 1 - Liverpool na Barcelona zinatamani kuipata saini yake.
 
Tetesi
ARSENAL WANAMTAKA FELLAINI


Arsenal wameugeuzia moyo wao kwa kiungo mahiri wa Manchester United Marouane Fellaini, Calciomercato limeripoti.
Mbelgiji huyo yupo kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake Old Trafford, pia amekuwa akiivutia Besiktas ya Uturuki.
 
Tetesi
ARSENAL WANAMTAKA FELLAINI


Arsenal wameugeuzia moyo wao kwa kiungo mahiri wa Manchester United Marouane Fellaini, Calciomercato limeripoti.
Mbelgiji huyo yupo kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake Old Trafford, pia amekuwa akiivutia Besiktas ya Uturuki.

Haaaa haaaa hii ni zaidi ya tetesi swahiba.
 
Arsene Wenger amedokeza kuwa anaweza kuhamia kwenye ukocha wa timu za taifa atakapomaliza kibarua chake Arsenal
Mkongwe huyo wa miaka 68 amebakiwa na miezi 18 kwenye mkataba wake Emirates na amekuwa akihusishwa na tetesi za kuinoa Uingereza.
Inafahamika kuwa Shirikisho la Soka Uingereza lilikuwa likitaka kumpa kibarua Wenger baada ya Roy Hodgson kujiuzulu kufuatia Uingereza kutolewa michuano ya Euro 2016, lakini Mfaransa huyo alitaka kuendelea na soka la klabu.
Inasadikika kuwa Paris Saint-Germain ndiyo klabu ambayo angeenda kuinoa ikiwa ataendelea na ukocha atakapoondoka Arsenal, lakini alipoulizwa kuhusu uwezekano wa timu ya taifa, alikiambia beIN SPORTS:
"Huenda, naam nitafanya kazi hiyo lakini kwa sasa napenda kazi za kila siku za maisha ya kwenye klabu.
"Ladha halisi ipo hapo. Wiki nne tano [kwenye michuano] ni uzoefu tofauti. Lakini naamini uzoefu wa kuinoa klabu ni kazi ya kila siku.
"Siwezi kuwa na nguvu za mwili kufanya hivyo kila siku, kwa hiyo naweza kufanya hivyo [kuinoa timu ya taifa].
 
North London Derby updates,Giroud ameumia goti akiwa timu ya taifa possibly hatocheza game ya jumamosi.
 
Back
Top Bottom