Wazo la kiufundi juu ya madai kwamba Arsenal wanataka kumsajili Dimitri Payet.
Payet leo hakuwa katika hali yake ya kawaida ile ya kupiga chenga za maudhi na kufungua vyumba kwa wachezaji wenzie.
Alianza mchezo kwa kumtumia vizuri mchezaji wa pembeni Manuel Lanzini lakini Lanzini na wacheaji wenzie hawakumshirikisha sana Payet hivyo kumuacha peke yake yaani akawa "isolated".
Lakini muda mrefu Payet akibanwa na khasa alipowekwa chini ya uangalizi na Granit Xhaka na kushindwa kufurukuta kabisa.
Lakini baadae alipoingia Andy Carroll ni pale alipopiga mpira wa adhabu na Carroll akauweka kimiani na hivyo kuwa ni "assist" kwa Payet.
Kwa kuwa Gabriel alikuwa akipanda mara kwa mara hiyo ndiyo ilikuwa nafasi ya pekee kwa Payet kuitumia kuisumbua ngome ya Arsenal lakini hakuwa na uwezo wa kubaini nafasi hiyo.
Je anaweza kuisaidia Arsenal?
Huku Santiago Cazorla akiwa majeruhi kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo, Arsenal wanaweza kujaribu kumsajili Dimitri Payet akiwa kama "attacking midfieder" kwa upande wa kulia.
Mesut Ozil leo alianza kwa kutoa pasi ambayo ilisababisha goli la kwanza kwa Arsenal. Lakini pia Alex Oxdale Chmbaerlain na Theo Walcott wote leo wameshiriki kwa ufanisi mkubwa kuchangia ushindi kwa Arsenal.
Hivyo pamoja na wachezaji hawa kuwepo bado wanasaidia sana kwenye eneo la kushambulia au attacking midfielders hivyo kufuta wazo la kumuhitaji Dimitri Payet ambae bado hajamfikia Santi Cazorla kwenye idara ya upishio wa vyumba na sahani za kufungia magoli kwa washambuliaji wake.
Uwezo wa kutoa pasi murua na mbinu za kutafuta kutoa pasi hizo ndiyo silaha kuu ya Santi Cazorla sifa ambayo Dimitri Payet hana.
Kwa hiyo basi, Arsenal hawana haja ya kumsajili Dimitri Payet na itakuwa ni upotezaji wa fedha huku Alexis Sanchez na Mesuti Ozil wakihitaji maboresho ya mishahara yao.