Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Hongereni Arsenal ... vijana wameonyesha game la hali ya juu na Porto walikuwa wamezidiwa. Hongera kwa kusonga mbele, kwa game kama la leo nadhani timu pinzani kwenye CL zinaweza kuwa na kiwewe.
 
Leo kweli kazi ipo. wangepigwa usingewaona humu kxenye thread yao.
au wangekuwa wanamlaumu wenger tu.

Hatuna kawaida ya kukimbia sisi bwana,wanaokimbia mbona wanajulikana aisee..tunakufa kijerumani...kila timu ikifungwa kocha ndo wa kwanza kuangaliwa aisee,yeye si ndo mwalimu....Tumeshinda 5-0,hata kama hampendi...lol
 
Bayern wamewatoa Fiorentina. Je, huu ndio mwisho wa Italian clubs?

Bado akina Milan wawili wanasubiri hukumu zao, mmoja kesho na mwingine wiki ijayo au tayari umeishazipa ushindi timu za Manure na Chelsea? Kwenye mpira wa miguu lolote linaweza kutokea, kwa hiyo tusubiri dakika 90 za kesho na nyingine 90 za wiki ijayo.
 
Hongereni kwa mara nyingine kupita, subirini tu draw ya next round.

Narudia tena...Tuko tayari kucheza na timu yoyote tutakayopangiwa....Hivi baada ya game ya Porto tulipofungwa 2-1 si kuna watu walisema kwamba safari yetu imewadia???,yako wapi leo...lol
 
Nimerudi daha vijana leo walikuwa ni noma hii ndo Arsenal sasa. Lile goli la Nasri ilikuwa ni balaa!
 
Bado akina Milan wawili wanasubiri hukumu zao, mmoja kesho na mwingine wiki ijayo au tayari umeishazipa ushindi timu za Manure na Chelsea? Kwenye mpira wa miguu lolote linaweza kutokea, kwa hiyo tusubiri dakika 90 za kesho na nyingine 90 za wiki ijayo.
Hapana chief, sijatoa hukumu bado. Nilikuwa najaribu kucheck kuangalia kwa miaka hii ya karibuni vilabu vya Italy vimekuwa vikifanya sio vizuri sana with exception of AC Milan, wakati vile vya England vimefanya vizuri. Tusuburi tuone kama history itaendelea kuwa hivyo.
 
Narudia tena...Tuko tayari kucheza na timu yoyote tutakayopangiwa....Hivi baada ya game ya Porto tulipofungwa 2-1 si kuna watu walisema kwamba safari yetu imewadia???,yako wapi leo...lol
Kina nani hao chief?!
 
Natumaini unakumbuka hapa ... .... ......

Cesc-Fabregas-Arsenal-Premier-League2_2401062.jpg



Je hapa ... ....


_47444008_nasri_getty766.jpg


Wapinzani wetu walie tu ... ...
 
lol basi leo hatulali humu..

Ni kweli hamtalala(hasa wewe),unayakumbuka maneno haya hapa chini baada ya game yetu ya kwanza na Porto...

haya;

'Naona nyie washabiki wa Arsenal na mie nimeshawazoea.

Safari yenu ya UCL mwaka huu umekuwa fupi zaidi. Porto gemu ya pili watarudi nyuma wote na itakuwa stalamate na mechi ya hovyo,. Na kwa sababu Arsenal huwa wanahamanika, watataka kwenda mbele kutafuta goli as a result watapigwa counter moja kule kule kwa Cliche na kaunta itazaa mtoto. Then it comes the usual part kuugulia maumivu. Poleni in advance.

Ila inashangaza kama kule Emerates kuna watu wenye akili timamu. Hivi kununua kipa mzuri kama Sorensen inaonekana kuna gharama kubwa zaidi kuliko kutolewa kwenye hatua za awali za FA Cup au UCL?? Nadhani kuna mahali jambo flani halipo sawa.'

na haya;

Nitarejea hapa siku ya mazishi kukwoti maneno yangu menyewe na kuyapigia mstari..he he he..

Naona leo ndo siku ya mazishi umerejea kukwoti maneno yako...Yanakushuka tu...lols
 
Arsenal boss Arsene Wenger on his side's 5-0 win over Porto, to seal a 6-2 aggregate victory: "It is never perfect but it was a very good, very strong performance. Our first half was excellent and then after a bit of a struggle at the start of the second half, Samir Nasri's brilliant goal settled us down and we were comfortable winners."

Well bado tuna kazi kubwa kwenye mechi zilizobaki, Fabregas apone haraka na majeruhi warudi upesi tumalize msimu kwa kishindo.
 
Kina nani hao chief?!

Abdulhalim na Masanilo....Angalia walivyosema hapa,nawakwoti

Masanilo:

'Poleni sana safari hii mnaishia round hii! Maana Emirates jamaa watapiga counter attack kupitia kwa Gael Clinchy'

Abdulhalim:

'...ambako hakatapatikana.

Arsenal haina historia ya kuperform under pressure.'
 
..leo naenda kuangalia kwenye Tv niachane na livestreaming hizi sometimes zinaleta kokoro!!
Jamani leo sitakuwepo kujadili mwenendo wa game dk kwa dk ila am going out to share na jamaa hii ya kuangalizia home inakosa mvuto sometimes

...that's what i did leo, kumbe wengi tulijichanganya 'pub' basi... 😀



_47442262_bendner466.jpg




Come on Nicklas Bendtner ... .... ....

Hao defenders wa Porto utumbo kabisa!

...si utumbo kaka, kuzidiwa, 😀😀😀

naona yule aliyeandika history ya porto kwamba hawajawahi kufungwa second leg baada kushinda first leg kaenda kufanyia editing post yake lol.

...aha ahaaha ahhahhaaaaa!, ama leo raha! 😀😀😀

Sie tunaenda kulala bana baada ya kushinda...Siku hizi tunashangilia kimyakimya...lol

....😀😀😀 kimya kimya tu zis dayzzzz, "Ssssshhhhhhhhhh...!" na wala mengi sintosema...".....,kwa mwerevu ni kicheko! "😀😀😀

BIG UP "Ze Gunners" wote, Big uppppppp!!!!!
 
Ila huyu kijana Song aisee ni balaa anauweza mpira huyu mtu bana
 
Back
Top Bottom