Wapenzi wa Gunners msiwe na wasiwasi,Wenger msmu ujao atakuwa busy sana.
Kuondoka kwa Flamini, Arteta na Rosicky ndio kutafanya Arsenal isajili wachezaji watatu.
Wachezaji hao ni wa sehemu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji.
Kampuni ya Collins Sarri Statham Invstiment ambayo ndio inashughulikia hesabu na akaunti ya Arsenal wamesema kwamba kiasi kilichopo kilichotengwa kwa ajili ya usajili kwa Wenger ni milioni 54.1.
Pia accountants hao wamesema ni lazima Arsene Wenger auze wachezaji ili aweze kuongeza fedha zaidi kusajili wachezaji atakaowahitaji.
Kuumia kwa Danny Welbeck kutafanya Arsenal itasajili mshambuliaji huku sehemu ya kiungo Granit Xhaka wa timu ya Borussia Monchenladbach ya Ujerumani inaaminika anamalizia taratibu za usajili utakaogharimu kiasi cha paundi milioni 33.8 hivi.
Pia Arsenal wanafanya utafiti wa kumsajili N'golo Kante wa Leicester ingawa Leicester wanaweza kuweka gharama kama milioni 20 hivi kwa mali yao hiyo endapo watashindwa kwa Granit Xhaka.
Hata hivyo Arsenal wana mtihani mkubwa wa kuchagua ni mchezaji yupi kati ya hawa ambae inamhitaji huku sehemu mbalimbali za maskauti wakimpa alama za juu N'golo Kante.
Hapo chini picha inaonyesha alama za ufanisi wa wachezaji hao wawili wakiwa uwanjani.
N'golo Kante
Granit Xhaka
Arsenal kama wanamtaka N'golo Kante itawabidi kufanya haraka na kulipa paundi milioni 20 ambazo zimo kwenye mkataba wake endapo utavunjwa.
Hivyo sehemu ya kiungo itakuwa na Mohamed Elneny, Jack Wilshere, Francis Coquelin na Santi Cazorla, huku Wenger akitaka mlinzi kuongo wa kusaidiana na Coquelin.
Theo Walcott huenda akasajiliwa na West Ham Utd kwa kiasi kama cha paundi milioni 20 ambazo zinaweza kutumika kumsajili beki mwingine.
Maskauti wa Arsenal wamerudi kuwatazama washambuliaji Alvaro Morata wa Juventus na Mauro Icardi wa Inter Milan kuanza utaratubu wa maulizo.
Mchezaji mwingine alieko kwenye ufutiliaji ni mshambuliaji wa Real Madrid James Rodriguez ambae amekuwa akikaa sana bench na aaweza kusajiliwa na Arsenal kwa malipo ya paundi laki 120,000 kwa wiki.
Walcott ambae hatarajiwi kuchezea timu ya Uingereza kwenye fainali za kombe la Ulaya ameshindwa kabisa msimu huu kuonyesha makucha yake na meneja wa Uingereza Roy Hodgson ameamua kumfikiria Andy Townsend.
Ntarudi baadae kuelezea ufuatiliaji wa Arsenal katika kumsaka beki mshahara mwingine.