Mkuu usiwe na wasiwasi Arsene Wenger anaweza kutumia hadi milioni 150 kufanya usajili ambao hajawahi kuufanya kwa misimu karibu mitatu iliyopita.
Suala la Leicester City kuwa mabingwa, Man City, Liverpool, Chelsea, na Man Utd kupata mameneja wakali limemuamsha sana, achilia mbali Southampton, West Ham na Swansea kuwa timu zinazotishia kushika nafasi nne za juu.
Richard nina wasiwasi sana na Madrid wale jamaa ni wafanya biashara watamrudisha Morata ila bei watakayo kuja nayo itakua kubwa sanaaa usishangae wakaanza above £40 million,ila ngoja tuone balaa lao na yule Higuain naona hanunuliki duh soko la washambuliaji limekua gumu sana sasa ivi viungo ndio wapo wengi sokoni.
Richard nina wasiwasi sana na Madrid wale jamaa ni wafanya biashara watamrudisha Morata ila bei watakayo kuja nayo itakua kubwa sanaaa usishangae wakaanza above £40 million,ila ngoja tuone balaa lao na yule Higuain naona hanunuliki duh soko la washambuliaji limekua gumu sana sasa ivi viungo ndio wapo wengi sokoni.
Ni kweli kabisa kwani Real watataka kuweka hata milioni 50 ili kupata faida kubwa wakifahamu kwamba kutakuwa na vita kati ya Arsenal, Man Utd, Chelsea na PSG kutaka kumsajili mchezaji huyo.
Lakini habari za ndani zinatoka zikidai kwamba Arsenal wamepania kuhakikisha wanamsajili Morata na wako tayari kuvunja mfumo wa mishahara.
Arsenal wanaweza kumlipa Morata 150,000 kwa wiki ikiwa ni tofauti ndogo na ile 140,000 anayolipwa Mesut Ozil amabyo nayo wanataka kumuongeza hivyo hawa wawili wanaweza kulipwa 150,000 kwa wiki.
Kama umefuatilia post zangu mwaka 2014 Arsenal walitaka kumchukua Morata kwa mkopo na yeye akakataa na kwenda Juventus.
Baada ya kufanya usajili wa Granit Xhaka mapema na kuzuia timu zingine zisimsajili mchezaji huyo, Arsenal sasa wameelekeza macho nchini Italy.
Nafasi ya ulinzi.
Arsenal wamemgundua mchezaji mkoba wa Napoli aitwae Kalidou Koulibaly kama mtu anaeweza kushirikiana vema na Boss (Laurent Koscielny)
Kaoulibaly ana umri wa miaka 24 na ni mzaliwa wa France anaweza kugharimu kama Euro milioni 26 hivi.
Pia katika eneo hili la sehemu ya ulinzi kuna wachezaji wengine kadhaa ambao wameangaliwa na maskauti akiwemo Lucas Hernandez wa Athletico Madrid, mkoba wa Celtic ya Scotland Kieran Tierney, mkoba wa Bolton Wanderes Robert Holding na Ryan Sessegnon wa Fulham.
Hali kadhalika yumo beki mwingine wa kati wa timu ya Velez Sarsfield aitwae Maxi Romelo.
Nafasi ya ushambuliaji.
Olivier Giroud na Theo Walcott wameipotezea Arsenal nafasi nyingi za kushinda mechi kadhaa muhimu katika msimu uliopita.
Na hata Danny Welbeck aliporudi kutoka kwenye majeraha ya gotihakuweza kucheza mechi nyingi kabla ya kuumia tena na sasa atakosa kucheza kwa zaidi ya miezi sita.
Hivyo bila shaka yoyote Arsenal hasa baada ya kumsajili Granit Xhaka bado wapo kwenye dirisha la usajili wakiangalia uwezekano wa kusajili mshambuliaji ambae yupo tayari kuleta tofauti.
Alvaro Morata ndie anaeongoza kwenye orodha akifuatiwa na mshambuliaji mwenzie wa Juventus Paulo Dybala.
Tofauti ya Alvaro Morata na Paulo Dybala ni kwenye kasi ya kushambulia ambapo Morata ni wa mtindo Olivier Giroud ambae anapoteza mipira na anapopoteza mpira huacha kuufuata lakini Morata huwa hapotezi mipira (ball control) na huweza kufunga kwa kila situation.
Alvaro Morata
Lakini wote hawa wawili wana uwezo mkubwa wa kupiga mashuti na kufunga na kwa sasa wao wanashindana katika first 11 ya Juventus huku Mario Mandzukic na Andrea Favilli wakiwa wanaanza kama wachezaji wa akiba.
Lakini meneja wa Juventus Massimilliano Allegri alianzisha mtindo wa kuzungusha muda wa uchezaji kati ya washambuliaji hawa wanne na kutokana na kila mmoja kutaka kucheza kwa muda anaopenda hii inaweza kuwa sababu ya Morata au Dybala kuamua kutafuta kuchezea timu ingine.
Paulo Dybala akijaribu kukabiliana na beki wa AC Millan ambae anatoka Colombia Cristian Zapata.
Uchezaji wa Dybala ambae ana miaka 22 ni mithili ya uchezaji wa Alexis Sanchez ambapo hupenda kusukuma nyuma mabeki na wakati huohuo kutafuta nafasi ama kwa wachezaji wenzake au yeye mwenyewe kufunga.
Vincent Janssen wa AZ Alkmaar ya Holland akifuatiwa na Sadio Mane wa Southampton na hawa ndio washambuliaji ambao hawaonei haya nyavu za timu pinzani.
Vincent Janssen
Vincent Janssen amefunga magoli 27 katika mechi alizochezea kwenye timu yake hiyo ya AZ Alkmaar yeye ana nguvu, uwezo wa kumiliki mpira na hukimbia kwa kujiamini awapo na mpira.
Lakini hawa wachezaji wote bado wapo kwenye utafiti wa kina ingawa Alvaro Morata anaongoza kwa kuwa mchezaji wa pili kuweza kusajiliwa na Arsenal.
Mkuu usiwe na wasiwasi Arsene Wenger anaweza kutumia hadi milioni 150 kufanya usajili ambao hajawahi kuufanya kwa misimu karibu mitatu iliyopita.
Suala la Leicester City kuwa mabingwa, Man City, Liverpool, Chelsea, na Man Utd kupata mameneja wakali limemuamsha sana, achilia mbali Southampton, West Ham na Swansea kuwa timu zinazotishia kushika nafasi nne za juu.
Bado mnakremu kuwa nafasi ya 4 ni ya Arsenal sio, endeleeni. Angalia rekodi lini tumemaliza nafasi ya 4..... Wengine tunawaona kumaliza ndani ya top 4 imekuwa mbinde in spite of spending £150 billions na wengine wameshindwa kumaliza in top 9 afu nasikia watasambaratika msimu ujao..
Usajili Updates: Real Madrid wawaambia Arsenal Morata atagharimu Euro milioni 49.
Klabu ya Real Madrid wamewataadharisha klabu ya Arsenal kwamba endapo watataka kumsajili mshambuliaji huyo bais utabidi watoe kiasi cha Euro milioni 51 au sawa na paundi milioni 38.
Lakini kabla ya Arsenal kumsajili mchezaji huyo itabidi Real wamsajili upya halafu wamuachie asajiliwe na Arsenal hivyo kupata faida ma mbili.
Alvaro Morata
Madrid wanaweza kumnunua Morata kwa Euro milioni 30 na kumuuza kwa Euro milioni 51 wanakuwa wamepata faida ya Euro milioni 20.
Klabu hiyo ya Santiago Bernabeu miaka miwili iliyopita ilimsajili Morata kwa gharama ya paundi milioni 16 na endapo itamchukua kutoka Juventus itapoteza kama paundi milioni 8 hivi, lakini kuweza kupata faida mara mbili ikiwa kalbu kama Arsenal watafanya biashara asubuhi na mapema.
Hivi sasa mshambuliaji huyo yupo kwenye mazoezi na timu ya taifa ya Spain kujiandaa na Euro 2016 na wiki jayo anatarajiwa kukutana na maofisa wa Real Madrid.
Ntakuja na habari zaidi za usajili.
Wakati huohuo kumefanyika mabadiliko ya namba za jezi za wachezaji na Aaron Ramsey amepewa jezi namba 8 ambayo ilikuwa ikitumiwa na Mikael Arteta.
Ramsey alikuwa akitumia jezi namba 16.
Namba hio 8 imewahi kutumiwa na wakongwe Ian Wright na Freddie Ljungberg.
Alexis Sanchez nae amebadilisha namba ya jezi na atavaa namba 7 mgongoni badala ya 17 na namba hiyo 7 ilikuwa ikitumiwa na Tomas Rosicky.
Alex Iwobi atatumia namba 17 ambayo ilikuwa ni ya Alexis Sanchez. Iwobi alikuwa akivaa jezi namba 20.
Hivyo Gunners mkiwatazama wachezaji hawa wawapo uwanjani basi Ramsey ni 8 na Sanchez namba 7 na Alex Iwobi namba 17
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.