Ni kundi gumu sana wamepewa Arsenal.
Lakini Borrusia Dortmund tumecheza nao mara mbili msimu ulopita ,na Galatasaray tulicheza nao fainali ya UEFA Cup mwaka 2000 na walitufunga na kutwaa ubingwa.
Ila nina wasiwasi na mpango mzima wa UEFA katika kupanga hii ligi.
Kwa mfano ndani ya misimu minne Arsenal inakutana tena na Borrusia Dortumund ya Germany mara tatu hivo hivyo ikiwa kwa Manchester City kwa Bayern Munich pia ya Ujerumani na CSKA Moscow ya Russia ambayo inacheza tena kwa mara ya pili.
Hali hiyo inaikumba pia Chelsea ambao watakutana tena na Schalke ya Germany.
UEFA lazima waangalie hali hii ya kuonekana kama wanapanga baadhi ya timu kucheza kwa pamoja ili kukwepana ili kutokuweza kukutana kwenye hatua ya mtoano.
Ukitaka kuangalia chunguza makundi A na B baadhi yao wtoe ni mabingwa katika ligi za nchi zao na kundi A ndio kabisa limepanga mabingwa wote. Pia kundi D nalo limetoa angalu bingwa kutoka kila nchi.