Ng'wanza Madaso
JF-Expert Member
- Oct 21, 2008
- 2,268
- 338
Babu kwani wao waweze wananini,na sisi tushindwe tunanini? uwezekano wa kuwafunga hawa Aston villa,Manure,Chelsea na Liverpool tunao. Kwani kwenye historia yetu hatujaweza kuwafunga? kama tulishawafunga kwa nini tushindwe sasa? Arsenal ni ile ile na kocha ni yule yule,babu tutawafunga tu usikate tamaa mapema.Naona wapanga ratiba waliamua kutumaliza wiki hizi mbili maana wametupangia vigongo vya mechi kitu ambacho si kawaida kabisa. Tukiweza kujipatia kati ya points nane na kuendelea basi tutaendelea kuwemo kwenye kinyang'anyiro cha EPL, vinginevyo tutakuwa tumeyaaga mashindano hayo.