Mkuu Belo na wengine hakuna shaka mimi nipo na ntakuwepo hapa Jumamosi mtanane utapoanza na Arsenal tunacheza na Crystal Palace, tena nyumbani Emirates.
Timu kwa hakika imekamilika isipokuwa sehemu ya kati kidogo panahitaji kijana mwenye nguvu ili kulinda ile "back four".
Kuna dalili kwamba Arsenal itajaribu kumsajili Cheick Tiote wa Newcastle United au tutaendelea kuwaangalia William Carvalho wa Luiz Gustavo wa Wolfsburg ya Germany na Benedikti Howedes wa Schalke ya Germany.
Kuna wachezaji wengine ambao nao wanaangaliwa kama beki wa kati Daniel Agger wa Liverpool, kiungo Adrien Rabiot wa PSG, na kiungo wa Shakhtar Donetsk Douglas Costa.
Mpaka sasa tumetumia kiasi cha paundi milioni 60 na hivi karibuni tumemruhusu TV kwenda Barca hivyo tumeingiza paundi milioni 15 zingine, hivyo tunaweza kuitumia.
Kwa wale wakuu mnaoweza kuhudhuria mechi ya jumamosi, bei ya tiketi ya chini kabisa ni paundi 27 a ya bei ya juu ni paundi 129.50
kwa kutegemea na daraja la mechezo wenyewe kuna madaraja matatu yaani (A, B, au C).
Daraja rahisi kabisa ni la C, na vti vya bei rahisi ni vile vilivyo nyuma ya goli au karibu na kibendera cha kona pale mwisho wa ngazi.
Tukutane hapa jumamosi, na tusisahau ku-charge simu zetu.
COYG!!