Jamani Gunners wenzangu na mimi nimekuja rasmi humu kuwaongezea nguvu dhidi ya makurumbembe kama Nzi, Ntuzu, Belo na Mentor nilikuwa viewer tu, nimeona kuna haja ya kuwa active.
kusindikiza sio, nilidhani huu wimbo uliisha May 20,2014 kumbe bado unaendelea lol . Man United mlifanya nini msimu uliopita kati ya Arsenal na Man United nani aliyeondoka mikono mitupu ? Tangu lini kubeba Kombe kukawa ni kusindikiza ?
Msimu huu tukiwafunga man utd tu ubingwa wetu.Hii mishetani imetutia gundu kwa kipindi kirefu sana.Na siku tukiyapiga bao nitawakojolea mashabiki maandazi wao wote.Nyambaf
Kesho shughuli ndiyo zinaanza rasmi. Shughuli ambazo huwaletea furaha kubwa sana wapenzi wa timu mbali mbali zinazoshiriki EPL na wengine kuwa na majonzi ya hali ya juu.
Usajili wetu wa mwaka huu ni mzuri ukilinganisha na wa zaidi ya miaka mitano iliyopita. Tukiweza kuepuka majeruhi ya kutisha na ya muda mrefu basi ngome za timu nyingi za EPL zitakuwa na kazi kubwa sana kuhakikisha nyavu zao zinakuwa salama kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara ya safu ya ushambuliaji.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.