Hello Gunner.
Hatimaye tumefika kileleni. Kazi iliyopo kwa sasa ni kuweka alama chanya ya mwisho katika ulimwengu wa soka kwenye FA Cup.
Tumejikongoja katika mechi hii lakini hatimaye uzoefu wetu katika medani ya mpira wa miguu umetufanya kufika kileleni.
Hakuna sehemu ya mchezo nisiyoipenda katika mpira wa miguu kama sehemu ya maamuzi kwa kupigiana penati. It was psychological torture!.
Kuna watu hapa kazi yao ni kulalamika tu. Kuna wengine bado wanalalamika kuhusiana na kikombe hiki pamoja na timu yetu kufika kwenye fainali ya FA Cup. Huwezi kulalamika kuhusu uchezaji wa timu kwenye kikombe cha FA CUP wakati timu iko kwenye fainali. Nitaelewa kama malalamiko yanatokana na timu kushindwa lakini siyo kufanikiwa kufika kwenye fainali.
Kwangu mimi sijaweka matumaini sana ya kuchukua kikombe hiki kwa sababu wiki tano kuanzia leo inaweza kubadilisha mambo yote kuhusiana na afya za wachezaji.
Tunawaachia football pundit uwanja wao. We don't care!. We'll back at Wembley on 17th May 2014 for the final.