Ubumuntu
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 14,382
- 10,951
Nadhani tunaitajika hata kuridhika na tulichopata maana nani alijua surprise ya babu wenger ni kutuletea Ozil tena kwa £ 42.5M ? Ukweli kwa sasa sio wakati wa kuokoteza wachezaji kwa timu kama Arsenal na ndio maana alimtaka Suarez mpaka alipoona Liverpool watamchelewesha ndio amemchukua Ozil kwa kuwa ni kama Bergkamp mpya,kwa kumpata Ozil tumefungua njia mpya kuwaleta wachezaji wazuri pia angalia suala la mshahara nao wachezaji hawatakiwi kupishana sana kiasi kwamba unaweza leta mgomo wa chini kwa chini nadhani babu anachotakiwa kuangalia ni suala la mishahara kwa wachezaji atakaowaleta na wengi wanataka mishahara mikubwa,kama uliangalia mechi na Tottenham tulimkosa mtu kama Ozil kuweza kumalizia ile mipira na kupata magoli mengi,na tushukuru kumpata Flamini kwa kweli amecheza kiungo ile ya Song maana tatizo la Arsenal lilikuwa ni Kiungo mkabaji anaejua kazi yake tuseme ukweli Ramsey na Arteta walikuwa wanajitahidi lakini sio kama anavyocheza Flamini
Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
Kwa hiyo kwa Ozil matatizo ya Arsenal yamekwisha? Kwa hiyo tutarajie ubingwa gani kutua Emirates mwaka huu?
Washabiki wa Arsenal, kweli washabiki maandazi!!
Alikuwepo huyo Song, Arsenal ilishinda nini?!? Alikuwepo Cesc, mliyemwona kama 'mungu mtu', mlishinda vikombe vingapi?!?
Hakuna ubishi kwamba Ozil ni mchezaji mkali sana, tena sana. Mimi namkubali sana Ozil na toka kabla hajaenda Real, nilitamani Man United wamchukue, lakini wakambwela.
Lakini kumpata Ozil na huyo pensioner Flamini, sidhani kama ndiyo matatizo ya Arsenal yataisha.
Anyway, nisijifanye naijua sana Arsenal. Tukutane Nov. 10 pale OT.