Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Asante mkuu....

Nilitaka Ndetichia anijibu maana tangu jana ameanza kutukana mamba kabla hajavuka mto....

Kaingia mwituni huyo maneno mengi kama pili pili manga imekula kwake, ngoja tuangalie tutapata wachezaji wangapi wapya kabla ya dirisha kufungwa. Theo leo amekuwa clinical safi sana.
 
Gedion Zelalem anaingia Ox anapumnzishwa ...... ...... ... .
ooops nachikia wanoko wanaulizana who are these
Gedion and Perez khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
watajijuu
Mkuu kuna watoto watatu wajerumani wenye vipaji vya hali ya juu ambao endapo hawatauzwa wataifanya Arsenal ing'are siku za mbeleni....Gnabry, Zelalem na Oisfeld....

Hawa watoto ni balaa....
 
Mpira umeisha Gunners 3 - 1 Man Shitty .... mambo yote chacha kwenye EPL na usajili wa vifaa vipya kama ikiwezekana.
 
Reactions: Mbu
........mmetulia kidogo?
Kelele mingi sana nyie wapiga bodi humu.....

Nxt Moyes nae tutampa ukaribisho kazini!!!!!

COYG, together we stand !!!!!
 
Isaac Hayden aliingia dakika za mwisho kabisa kuchukua nafasi ya Ramsey nangoja kuona moto wa hawa watoto. Wacha wapate experience ili wakihitajika wacheze.

Kwa wanaotaka kuiona hii mechi kama ilivyochezwa waingia hapa .... ... Arsenal.com then wachague player
 
Naona na Giroud anaanza kurudi kwenye form. Sasa hiv anapiga magoli ya kwenye PS....am happy for him
 
GIDEON ZALALEM is Fabregas and Xavi and Iniesta rolled in one, dogo ni new Zidane uwezo wake wa mapishi balaa kama akina Stoke hawatovunja mguu dogo ata-shine sana. Very excited with new season.

Mkuu hawa vijana wamefurahisha jinsi walivyo wepesi na wana stamina.

Hata hivyo mzee Wenger amesema kwamba kikosi hiki hakiwezi kuhimili mechi 55 kwa msimu mzima, kwahio kuna wachezaji kadhaa wataongezwa kuanzia wiki ijayo.

Tunaweza kumsajili Luiz Suarez paundi 160,000 (kwa wiki) na Luiz Gustavo kutoka Bayern Munich kwa kiasi kati ya 60k - 70k kwa wiki gharama za hawa zinaweza kuwa kama paundi 86,000 peke yake.

Wenger amewaambia wazee wa "board" kwamba ni lazima aongeze wachezaji, kwahio tusubiri.


Luiz Gustavo

Mchezaji huyu wa kiungo wa kimataifa ana umri wa miaka 26 na asili yake ni Brazil. Amechezea timu ya taifa ya Brazil mara 10 na mara ya mwisho alicheza kwenye Confederations Cup.

Anaweza kucheza kwenye nafasi ya ulinzi au kiungo.

Maskauti wa Arsenal wametathmini ni wachezaji wangapi wa kiungo waliopo pale Bayern na inaonekana wana wachezaji zaidi ya saba ambao ni Franck Ribery, Javi Martinez, Mario Gotze, Bastian Schweinsteiger, Arjen Robben, Toni Kroos na Xherdan Shaqiri na wote hawa wanashindania nafasi ya kucheza ukimjumlisha Thiago Alcantara ambae amejiunga kutoka Barcelona mwezi July.

Bayern Munich ilimsajili mchezai huyu kutoka timu ya Hoffenheim kwa Euro milioni 10.

Tokea meneja mpya Pepe Guadiola aanze kuifunza timu hiyo ya Bayern yanye makao yake makuu yajulikanayo kama Allianz Arena, Gustavo amekuwa anakosa kucheza kwenye timu ya kwanza na hivyo kuwa na wasiwasi juu ya nafasi yake kwenye timu ya Brazil itakayocheza kombe la dunia mwezi juni mwakani.

Ikiwa utakubali offer ya AFC basi Gustavo karibu Emirates.

COYG!!!!!
 
GIDEON ZALALEM is Fabregas and Xavi and Iniesta rolled in one, dogo ni new Zidane uwezo wake wa mapishi balaa kama akina Stoke hawatovunja mguu dogo ata-shine sana. Very excited with new season.

Kwa kusifia hivyo vitoto vyenu hamjambo, ila elewa kuwa Xavi atabaki kuwa kuwa Xavi tu the same as Iniesta. Zidane huo ulikuwa mtambo mwingine katika wachezaji waliokuwa bora duniani ukiwarank Zidane yupo nafasi za juu sana huwezi mlinganisha hata na Ronaldo.
 

Tumeisha wazoea nyinyi mashoga mlikuwa mnamwita Judas Van Purse na Cesc mlikuwa mnamdharau lakini ndio wachezaji ambao mnawalilia chacha .... ... grow up! last week mlivyokung'utwa kama gunia hukuonyesha pua hapa chacha leo ukelele mwingi kama wa Pinocchio. Khe khe khe khe khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
 
........mmetulia kidogo?
Kelele mingi sana nyie wapiga bodi humu.....

Nxt Moyes nae tutampa ukaribisho kazini!!!!!

COYG, together we stand !!!!!

Upo besti, mmefurahi wenyewe kushinda? Finally...EPL hiyoo tuanze kushambuliana!!
 
Mfarisayo kila kitu kina zama zake walikuwepo akina Pele, Cruyff, Platini, Eusobio wakaja akina Maradona, Gullit, Weah na tukashuhudia generation ya akina Zidane na Ronaldo na kufuatia akina Messi na Xavi so mkuu naelewa Xavi atabaki Xavi na Zidane atabaki Zidane lakini mark my word.....Kwa kijana wa miaka 16 huyu kijana ana exceptional footballing brain way ahead of his age....hebu basi muangalie kwanza mkuu hata youtube utakubali kwamba huyu ni special talent. Give credit where the credit due mkuu.
 










Cannibal Luis Suarez should be able to bite his way out of Anfield.
 
[h=5]Mpira wa siku hizi kwenye kiungo hauitaji sana kiungo mwenye kutumia sana nguvu kama zamani wakati vilabu vinatumia 4-4-2 kwani ili washambuliaji wawili wa relax timu iliihitaji Dm mwenye mapafu ya mbwa "anchorman" lakini Modern football imebadilika sana hiyo ebu tizama mifumo kama 4-3-3, 4-2-3-1 au 4-3-2-1 inahitaji full backs wapande zaidi kusaidia mashambulizi na mawinga wote wanakuwa kama viungo maana wanaweza kubadilishan positions wakati game ikiendelea ISIPOKUWA CF pekee yake

hapa unaweza kucheza na kiungo mkabaji ambae ni "good passer" hata kama hatakuwa na nguvu saana ali mradi viungo washambuliaji wajitahidi kukaba na kutopoteza mpira ovyo...mifano hai Manchester united msimu uliopita walikuwa na Michael carrick ambae kwangu mimi ni player of the season kwo manure, jana game yao ya community shield alikuwa tena man of the match na mchezaji Sergio busquests..kama mzembe hivi lakini ni fundi na ni mzuri sana kwenye kutoa pasi haraka kwenda department zingine ndio maana walimuuza yaya Toure kirahisi....

lakini kama timu yatumia 4-4-2 hapo lazima muwe na mvulugaji pale mbele ya mabeki...ila kwa vyovyote iwavyo kwa mifumo wanayotumia Arsenal ya sasa hakuna wachezaji wanaojituma kwenye game kama Aaron ramsey na Laurent koscielny na kusema ukweli sioni ramsey akikaa benchi hata siku moja kwa form aliyonayo na work rate yake, na Arteta ataendelea kuwa DM kama Gustavo akinunuliwa nahisi ni cover up na kuwa versatile inapobidi hata kucheza kama beki wakati flani....HONGERA SANA RAMSEY[/h]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…