Team News
Mikel Arteta hatacheza leo kutokana na kuwa majeruhi, na Jack Wilshere atacheza badala yake ingawa itabidi adungwe sindano ya kuondoa maumivu.
Olivier Giroud nae anarudi kwenye timu akiwa amemaliza kifungo cha mechi tatu baada ya kupewa kadi nyekundu kwenye mechi na QPR.
Newcastle wana majeruhi wengi sana Cheick Tiote ambae anaweza kucheza baada ya kuumia msuli na wengine Davide Santon, Steven Taylor, Moussa Sissoko, Massaido Haidara, Ryan Taylor, Haris Vuckic , kipa Tim Krul na mshambuliaji Shola Ameobi.
Hivyo kama Giroud ataanza basi Lukas Podolski nae atapisha na timu itakuwa na Szczesny, Sagna, Gibbs Mertesacker na Koscielyn, kiungo- Wilshere, Ramsey na Rosicky mbele yao na kwenye ushambuliaji ni Giroud na Walcott.
Au Rosicky anaweza kumpisha Podolski na akaja kipindi cha pili.
Kwa upande wa safu ya mabeki nadhani hakuna mabadiliko labda mtu aumie kabla mpira haujaanza.