Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Muda wowote kutoka sasa,beki wa kushoto wa malaga Nacho Monreal 26yrs atatua emirates kwa dau la pauni milioni 10,stay tuned!
Zaidi ya huyu ni mchezaji gani mwingine tunamfukuzia?
 
Bila Gibbs kuumia nadhani tusingesajili. Yule Diame hata ku-bid tumeshindwa?

Hatuko serious kweli nia yetu kumaliza wa nne.
 
Timu ya Arsenal jioni hii imekamilisha taratibu za kumsajili beki wa kushoto Nacho Monreal kutoka Malaga ya Spain.

Nacho ambae ana umri wa miaka 26 alikuwa tayari kwa ajili ya usajili wa mwezi Julai mwaka huu lakini kutokana na majeruhi aliyoyapata Kieran Gibbs imebidi usajili ukamilike leo hii.

Mchezaji huyo ambae pia huchezea timu ya taifa ya Spain amesajiliwa kwa mkataba wa miaka mitano utakaogharimu kiasi cha paundi 55,000 kwa wiki,na gharama zote za usajili zimefikia kiasi cha paundi milioni 9.


Nacho Monreal

Nacho anakuwa mchezaji wa pili wa Arsenal kutoka timu hiyo ya Malaga baada ya Santiago Cazorla ambe alisajiliwa mwezi July mwaka jana. Hata hivyo Nacho hataweza kucheza CLkutokana na timu yake ya Malaga nayo kucheza michuano hiyo.

Habari ingine nzuri ni kwamba Nacho anaweza kucheza mechi ya Jumamosi dhidi ya Stoke City.

Angalizo:

Arsenal watatangaza usajili wao siku ya Ijumaa.
 
Muda unakwenda na ikiwa timu iliyoweka bid kwa West Ham juu ya Momo Diame ni Arsenal basi hatuhitaji tena mchezaji hadi July.

Diame analindwa na kifungu kwenye mkataba kinachomruhusu kuzungumza na timu yoyote itakayojitokeza kuulizia kuhusu kifungu hicho ambacho kina kama paundi milioni 3.5 hivi.

Timu ya Arsenal imekuwa ikihusushwa na usajili wa mchezaji huyo anaejulikana kama "Midfield General" kwa wapenzi wa West Ham.

Kama West Ham watakubali deal hilo basi Diame atakuwa ameondoka kwenda kwenye timu mpya kabla ya saa tano ya usiku kwa saa za UK.
 
gun__1359624621_giroud_liverpool.jpg



Going for grory ... ... ... ..

Wakuu msiwe na wasi wasi, mwaka wa shetani huu hakuna timu ambayo haivujishi magoli hata wale wanaojisifia ni kwa sababu ya kubebwa bila hivyo si chochote wala lolote. Tusubiri Prof atakuja na kifaa gani. COYG

 
Wakuu mpoo!

Muda unazidi kuyoyoma na mambo bado kimya.

Mzee Wenger hataki kabisa habari yoyote ile kuvuja.
 
Mjue Nacho Monreal.

Nacho+Monreal.jpg

Nacho Monreal

Ni beki wa asili wa kushoto tofauti na wachezaji wengi wa pembeni ambao hubadilishwa kwenda kucheza kama mabeki wa pembeni.

Mchezaji huyu wa kimataifa wa Spain alianza kwa kuchezea timu ya Osasuna kablaya kuhamia timu ya Malaga ambayo mwaka huu inashiriki kombe la klabu bingwa Ulaya.

Ana sifa zote za kuwa beki, ana nguvu na anaposimama nyuma na mabeki wenzie huleta uwiano wa kukabiliana na timu adui. Pia hupenda kupanda na kushuka na hutumia akili sana kuwasoma washambuliaji wa timu adui.



Nacho+Monreal.jpg


Karibu beki mshahara Nacho kwenye timu yetu ya Arsenal.
 
Back
Top Bottom