Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Haya mabadiliko inaonesha wenger anataka kulinda hilo goli moja.

Goli moja halitoshi dakika hizi tunaweza kusikia draw
 
hii gemu leo tumetoka kwenye kisu tulikuwa tayari
AW sijui anajua wakti anabadilisha mchezaji kwa ajili ya nini?
 
Gunner mmoja humu ndani anapenda kutumia usemi "mdogo mdogo mpaka kileleni......."

Ndo hayo.. Sie ndio washabiki Wa kweli Wa soka bana, timu kucheza vibaya mechi 2 tatu na kuanza kutafuta mchawi (Kama chelski..!) sie Kawaida yetu, you stick with ur beloved team through thick and thin...

enhee tunasubiri wajao, naona nafasi ya 2 Kama inatuita vile.....!
 
Kipindi hiki kigumu sana EPL kutokana na sikukuu na hali ya hewa ya UK isiyoeleweka kama wanasiasa wetu uchwara wa bongo.

Sishangai MAN UTD wanaongoza ligi na lazaidi watu watasikitika sana baada ya matokeo ya leo usiku ya EPL

Walitegemewa kuwa vibonde wamevimba leo na makipa wamegoma kuokota mipira nyavuni kabisa
 
Wale tuliowapiga tano epl basement boys reading anawatoa kamasi watu wazima
 
January tujiongezee hata majembe mawili tu,striker mlafi na DM mpenda sifa.
 
Ba kuja arsenal for me itakuwa dream come true.. mkuu Stephan nsunzu definitly atakuwa a.goner soon... At list tunarudisha.Ile arsenal ya blacks.wenye nguvu sio kina djrou

Inaonekana Wenger anataka washambuliaji wawili au mmoja, na wa pembeni pamoja na kipa.

Ila ni lazima amuuze Chamakh na pesa imnunue Demba Ba au amsajili Davidi Villa wa Barcelona kwa mkopo. Halafu pia inabidi amuuze Andrei Arshavin ambae amekataa kwenda Zenit St Petersburg ya Russia.

Ikiwa Theo Walcott ataondoka mwezi ujao basi Winfred Zaha atasajiliwa ili kuziba pengo la Walcott lakini pia kuziba pengo la Arshavin endapo yeye Arshavin atapata timu mwezi January na Walcott kuamua kubaki ili aondoke mwezi wa saba mwakani.

Halafu kwenye makipa Chezzer anahitaji ushindani na hivi karibuni kuna magoli ya ajabu ajabu ameyaruhusu, kwahio huenda akasajiliwa kipa mwingine ambae inasemwa ni Mbelgiji Simon Mignolet kutoka Sunderland. Tayari Fabianski na Vito Manone wameambiwa tafute timu mwezi January.

Kwahio tutulie tu kuna usajili kabambe unaandaliwa na Wenger ambae amepanga kufanya mambo ambayo hajawahi kuyafanya kwa miaka yote 16 aliyokaa Arsenal.

NB:
Chezzer ni jina la utani la golikipa Wojciech Szczesny.
 
mtotowamjini said:
gooners mnataka players ambao hata hamjui wanachezea team gani :biggrin1: kaaazi kweli kweli

Punguza kiherehere mtoto.....Yaani wewe kila post ya Gunners lazima uiquote?.....

Hiki kwetu Tinde tunakiita ni kimbelembele cha MWAJUMA......

'Ya Ngoswe, muachie Ngoswe' bana......
 
Back
Top Bottom