Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

kweli mpira ni biashara lakini pia tizama wateja Arsenal ikishuka daraja wateja watapungua na wachezaji pia hawatokubali kuja Arsenal
 
Mkuu mie nimeshapoteza imani siku nyingi sana na AW na management yote ya Gunners. Walinimaliza nguvu kabisa pale walipoamua kumuuza Van Puuuu.... kwenda MANU. Makosa kama hayo ya kumuuza mchezaji wenu star kwa timu ambayo iko EPL hata siku moha SAF huwezi kumsikia akiyafanya. Nakumbuka miaka michache iliyopita Rooney alitingisha kibiriti na kutaka kuondoka MANU. SAF hamkutolea uvivu na kamwambia una uhuru wa kuondoka tutakuuza katika timu yoyote ambayo itatupa pesa nzuri lakini ujue timu hiyo haitakuwa UK bali ni nje ya UK kwa maana nyingine kuhamia katika ligi ya Germany, Spain, Italy etc Rooney mwenye akanyoosha mikono juu na kutia wino ili kubaki MANU.

Timu inashuka hadhi taratibu na ilhali Bank account ya Gunners imenona vibaya sana. Wanataka wachezaji wa bei poa matokeo yake one of the mighty team among the best teans in EPL, Europe and the World sasa hivi imekuwa kibonde cha hali ja juu. Siku hizi nikiangalia mechi najua uwezekano wa kwanza ni kufungwa, kutoa draw au tukibahatika kushinda kimanati manati.

Wachezaji pamoja na kulipwa mabilioni lakini nao wanataka kubeba makombe mbali mbali ya EPL, FA, UEFA etc lakini timu yetu ya Arsenal kila mwaka nafasi ya kufanya hivyo ndio inazidi kututupa mkono. wachezaji wa zamani wa Gunners wamejaribu sana kuongea kwenye vyombo vya habari mbali mbali kuhusu umuhimu wa kuwa na wacheza ambao wana experience ya kutosha lakini management ya Gunners imetia pamba masikioni huku timu ikizidi kudorora msimu hadi msimu.

Sasa hivi hata kuwapata wachezaji wakali duniani itakuwa ni kazi mno!!! maana inaonekana Gunners haiwajali hata masuperstar wake mbali mbali na hivyo kuhakikisha inafanya juu chini ili kutowapoteza na hivyo kujenga timu imara ya kuweza kupambana na MANU, MANC, BARCA, RM etc..Siku hizi hata tukicheza na vibonde wanajua hawa Gunners ni vibonde wenzetu tukikaza msuli basi tunaweza kuondoka na 3 points!!! :target::target:

Nitafurahi kuona mechi za nyumbani za Gunners uwanja unakuwa mtupu hivyo kuwapa mstuko mkubwa owners na management in order to kick them where it hurts the most, Gunners' bank account...labda ndio watatia akili kichwani na kuirescue timu kabla haijashuka daraja. Na kwa matokeo ya hivi karibuni sitashangaa kusikia Walcott naye ameamua kuvua jezi na kwenda MANC, MANU au Tottenham... nasubiri kwa hamu mchapo mkali wa J'pili kati ya MANU na MANC

Msema kweli....

Mkuu BAK hapo umenena., hilo ndio tatizo la AW na bodi yake. Na kama itaendelea hivi soon mtaanza kuuza na mashabiki, yangu maEyes.:glasses-nerdy:
 
jamanii goners .. match day! muhimu hiiiii vijana wanahasira
 
timu iko tayari wasiwasi wangu Ramsey lazima acheze Wenger atamuingiza tu kipindi cha pili
yule dogo hata akiwa bench mimi hua nina wasiwasi
 
Back
Top Bottom