Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Arsenal (The Gunners) | Special Thread

Viper kashengo wakati season inaanza walikua wanatucheka man utd tulivokua tunaachia magoli eti wenyewe wakawa wanasema wana strong defence hawaachii magoli wanashinda 2-0 1-0 au wanatoa draw 0-0 mi nilikua nawacheki tu na niliwaambiaga kua nyie nguvu ya soda its just a matter of time mtaanza kuachia and boy was i sooo right :biggrin1:

Timu ilikuwa ina defend vizuri tatizo kuna rift kati ya Bould na Arsene juu ya tactics huyu babu anapenda Attacking football na ki ukweli amekuwa rigid sana na mbinu zake zimekuwa zinatabirika sana na West bromwich Albion watatupa tabu next weekend

babu akubali kuwa modern tactics zimemshinda kbsaa na amebaki na Excuse kama mwanasiasa! Napenda mashabiki wanavyompa presha aone ile timu sio ya baba ake au ya kwake ameikuta...we need another manager with more ambition
 
Last edited by a moderator:
Viper kashengo wakati season inaanza walikua wanatucheka man utd tulivokua tunaachia magoli eti wenyewe wakawa wanasema wana strong defence hawaachii magoli wanashinda 2-0 1-0 au wanatoa draw 0-0 mi nilikua nawacheki tu na niliwaambiaga kua nyie nguvu ya soda its just a matter of time mtaanza kuachia and boy was i sooo right :biggrin1:

TULIA WEWE! HATA CHRISTMAS BADO MANURE URINATED MNAANZA KUFURAHI ....


28742_451355994921967_587920896_n.jpg

 
article-2241619-164C9587000005DC-49_634x419.jpg


Faida kwa wamiliki.

article-2241619-164D3C2E000005DC-223_634x471.jpg


article-0-164D4B45000005DC-285_634x341.jpg


Fedheha/maumivu kwa wachezaji.

article-2241619-164C919F000005DC-775_634x415.jpg


Kwa washabiki: uchungu, maumivu, na hali ya kujisikia kusalitiwa!

article-2241503-164CEC2F000005DC-71_634x400.jpg


Babu anaamini bado anajua kuliko hawa wote. Anaomba uvumilivu zaidi na zaidi!
 
arsenal imekua kichwa cha mwendawazimu , Yaani tokea mashabiki walikua wanaandika in Wenger we trust mpaka sasa ni full kuzomea

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
kama unaeza amini Arsenal ina wapenzi wengi kuliko timu nyingi kwani angalia hii thread ilivo na wachangiaji wengi kama wewe hii timu ikiwa inaendeshwa vizuri basi karibu ya wote ya wachangiaji watarudi,
Angalia wachezaji waliotoka karibia ya wote bado wana mapenzi na hii timu isipokuwa kuna kitu humu ambacho bado hajatokezea wa kumfunga paka kengele Tukubali kuna siri ndani ya Arsenal ambayo karibu itatolewa na ndio tutajuwa ni nini tatizo
Sijawahi kuwa fan wa Arsenal, he he..presha za nini?!! poleni sana
 
Yaani watu bado wanakijadili hiki Kitimu Kidogo cha Washika Bunduki? Aseno ni Kama Coastal Union tu kwa Tanzania
 
Wakulu mambo vipi,


Kuna wale wapenzi ambao hudhani kwamba baadhi yetu huwa tunakimbia hapa jukwaani, jibu ni hapana.

Mimi kwa upande wangu huwa sikimbii hapa jukwaani bali huwa naingia uwanjani kushuhudia mwenyewe mechi za timu yetu.

Kwa kweli matokeo ya jana yameniacha na maswali juu ya maamuzi au judgement ya Wenger kuhusu usajili, upangaji na matatizo ya majeruhi kwa baadhi ya wachezaji wake ambao huonekana ndio wachezaji muhimu kwenye first XI yake.

Nimegundua kwamba Wenger anacheza kamari katika uendeshaji wa timu yake ikiwapo uwanjani.

Ntaelezea baadhi ya michezo yake ya kamari kwenye maeneo mbalimbali ya timu yake.

Kipa:

Hili eneo Wenger amekuwa hajaweza kusajili golikipa imara langoni na Wojciech Szczesny inasemwa kwamba wiki karibia sita sasa amekuwa akitumia dawa za kutuliza maumivu na kucheza hivyohivyo. Szczesny ni kipa mzuri lakini amekuwa akipata maumivu mara kwa mara.

Lukasz Fabianski nae bado ni majeruhi na huenda asicheze kabisa msimu huu. Kwahio hali hii inaiacha timu bila kipa namba 1 na namba 2. Ingawa kuna kipa namba 3 Vito Manone ambae atabaklia kuwa kipa namba 3 na hata uwezo wake ulijaribiwa katika mechi za mwanzoni mwa ligi lakini kutokana na mabeki kutojipanga vizuri Manone hajakaa vizuri.

Wenger ameacha kumsajili Julio Cesar kutoka Inter Milan ambae ameishia timu ya QPR, Alan McGregor kutoka Rangers ya Scottland timu ilipatwa namatatizo ya kifedha jambo ambalo lisingekuwa tatizo kwa Arsenal. Kuna kipa kama Jussi Jääskeläinen wa Bolton ambae amekwenda na timu hiyo daraja la pili, Paddy Kenny wa QPR ambae amekuwa kipa namba 2 wa timu hiyo.

Hawa makipa wangesajiliwa kama cover kwa namba 1 na 2 Arsenal isingemtumia Szczesny akiwa anacheza na maumivu bali ingesajili makipa wazoefu wenye ujuzi, hivyo kamari hii ya Wenger imefeli.

Beki wa kushoto:

Kieran Gibbs ndie beki wa kushoto wa Arsenal namba 1 na anapoumia, Santosa huchukua nafasi yake, lakini Santos hatazamwi kama beki imara sana. Katika mechi ambazo Arsenal imecheza bila Gibbs imekuwa ikipata shida sana kiuchezaji maana Wenger anaamua kumtumia Vermaelen kama beki wa kushoto na kwa kuwa Vermaelen si beki wa asili wa nafasi hiyo, anakuwa anachanganyikiwa na ndio mechi na Fulham magoli yakarudi.

Watani wetu Man U walipomuachia Fabio akacheze kwa mkopo kwenye nafasi ya beki wa kushoto pale QPR wakawa wamebaki na Patrie Evra lakini wakaenda kumnunua dogo aitwae Butner ambae huwa anacheza pale Evra anapokuwa majeruhi.

Kwahio hapa tena Wenger amekosea kwa kutomsajili mtu kama Leighton Baines wa Everton ambae angekuwa ama beki wa kushoto au kucheza pale Gibbs anapokuwa majeruhi, hivyo karata hii ya kumtegemea Vermaelen kama beki wa kushoto pale Gibbs anapokuwa majeruhi imefeli.

Sehemu ya kiungo:

Baada ya kumuuza Alex Song kwa Barcelona, Arsene Wenger angeingia benki na kutoa hundi ya kununua mchezaji wa aina ya Marouane Fellaini au angeongeza dau kwa Nuri Sahin ambalo lilikuwa likihitaji kusema iwe ni manunuzi kabisa na sio mkopo (kwa Sahin) na pia angedharau wasiwasi wa tabia ya ugomvi wa Yann M'Vila ambae ni mtukutu awapo nje ya uwanja.

Mzee Wenger akatia karata zake za kamari kwa Abu Diaby ambae inajulikana historia yake ya kuwa majeruhi pale anapopigwa kiatu cha uhakika. Na ni9 mechi na Liverpool ndio Diaby alionyesha kwamba akiwa mzima anawezakufanya vitu vya uhakika na baada ya hapo amerudi meza ya majeruhi.

Arsena haina mchezaji imara wa katikati wa kulinda ile "back four" na ukiangalia goli la kwanza utaona Michu akichukua mpira kabla ya kufunga hakuzuiwa na mtu yoyote. Na ni jana Wenger ameona umuhimu wa watu kama Gilberto au Makelele wa Chelsea. Huku tena ni kufeli kwa kamari za Wenger.

Nafasi ya mshambuliaji:

Wenger alipomuuza RVP alipaswa mara moja azibe nafasi kwa kumsajili mshambuliaji makini ambae angeweza kufunga magoli ya uhakika. Wazo la awali la kumnunua Giroud lilikuwa ni kwa kucheza kama mchezaji wa akiba kwa namba 9 wa first XI ambae angekuwa labda ni Llorente au Cavani.

Tokea Giroud aanze kucheza amefunga magoli 4 kwenye mechi 14 wakati RVP akiwa Man U amefunga magoli 10 kwenye mechi 15 ambazo amekwishacheza.

Pia Wenger anacheza karata ingine kwa kuwachezesha Podolski na Gervinho kwenye nafasi ya mshambuliaji namba 10 jambo ambalo jana limejionyesha kwamba halifai kwani pale anapoamua kumchezesha Giroud kama namba 9 basi Podolski na Gervinho ni mmoja wao tu ndie acheze kama namba 10 au 11 na sio wote maana wanakuwa hawajui wanafanya nini uwanjani na Gervinho jana amepoteza nafasi nyingi sana kipindi cha kwanza.

Kuna washambuliaji ambao wana uzoefu wa kimataifa na hasa kwenye ligi ya Uingereza kama Kevin Mirallas au Steven Fletcher wa Sunderland, Dimitar Berbatov wa Fulham na Jermain Defoe wa Tottenham Hotspurs. Defoe alikuwa akitaka kuhama timu ya Spurs na kama Arsenal wangemnunua akawa "first striker" basi angeleta ushindani maana angechezeshwa na Podolski na Giroud akawa anajifunza namna ya kumalizia mipira wavuni.

Kitendo cha Wenger kuamua kutosajili mshambuliaji na kutupa karata zake na kuamua kumtumia Olivier Giroud kama mshambuliaji na Gervinho na Podolski wawe wasaidizi wake, ni kamari ingine iliyofeli.

Sasa wapenzi wa Arsenal tunasubiri kuona kwamba Arsene Wenger anarekebisha makosa yake na kununua wachezaji namba moja katika maeneo niliyoyaongelea na ni hapo tu ndio Arsenal inaweza kushinda mechi zake za mzunguko wa pili.
 
kama unaeza amini Arsenal ina wapenzi wengi kuliko timu nyingi kwani angalia hii thread ilivo na wachangiaji wengi kama wewe hii timu ikiwa inaendeshwa vizuri basi karibu ya wote ya wachangiaji watarudi,
Angalia wachezaji waliotoka karibia ya wote bado wana mapenzi na hii timu isipokuwa kuna kitu humu ambacho bado hajatokezea wa kumfunga paka kengele Tukubali kuna siri ndani ya Arsenal ambayo karibu itatolewa na ndio tutajuwa ni nini tatizo

Unajipa moyo kwelikweli mkuu.. Haya wee, ingekuwa idadi ya washabiki inatwaa vikombe mngeshinda..!!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Yaani watu bado wanakijadili hiki Kitimu Kidogo cha Washika Bunduki? Aseno ni Kama Coastal Union tu kwa Tanzania

Pengine unaangalia small picture .. ...Timu ambayo ni headlines kila siku, sio timu ya vichochoroni, Gunners under the city ni imara na dira yake inaangaza kona zote za ulimwengu, kama huwezi kufungwa basi wewe sio mshindani, ni Arsenal pekee ambayo iliweza kutwaa ubingwa bila kufungwa chini ya prof. , chacha njomba kama hii ni timu ndogo unafanya nini kwenye hili jukwaa? Au ndio kuweweseka kwenyewe ... ... Timu ambayo imefungwa magoli mengi hadi hivi sasa kwenye EPL sio Arsenal na EPL bado mbichi kabisa wala hatuna wasi wasi .. .. .stay tuned J4 tunakwenda kwenye CL hao Swan tutakwenda kuonana nao kwao, tutaona kama wanafahamu kitale au ilikuwa bahati nasibu .. ... ..

Prof knows wala isikupe shaka, yupo pale kuona mambo yanakwenda mswano na ndio anawanyima usingizi hadi mkome ... ... .. khe khe khe khe kheeeeeeeee you can't buy class. Ndio EPL hiyo kama huwezi mikiki mikiki yake kaa pembeni mahesabu mwezi May mwakani.

 
BJ timu yetu ina matatizo makubwa sana. Haiwezekani upoteze wachezaji wazuri katika misimu mitatu/minne iliyopita VP, Adebayo, Fabregas, Kolo Toure, Gael Clichy and Samir Nasri, Song na kisha wale wapya wanakuja na viwango vya chini zaidi kuliko wale walioondoka. Management yote inabidi ifukuzwe ili kuleta mabadiliko ya kweli vinginevyo kuna hatari kama si msimu huu basi ujao timu ikashuka daraja. Inauma sana kuona timu ambayo ilihitaji wacheza wazuri watatu au wanne miaka michache iliyopita kuongeza nguvu na kujiweka katika nafasi nzuri ili kuweza kutwaa taji la EPL na UEFA sasa hivi inaporomoka katika kasi ya kutisha. Chezea ubahili weye!...


Unajipa moyo kwelikweli mkuu.. Haya wee, ingekuwa idadi ya washabiki inatwaa vikombe mngeshinda..!!
 
BTW Chairman wa Gunners amepata mshituko wa moyo hospitalini (76 yrs old) ambako alilazwa kuanzia ijumaa ... ... ... ..more on Gunners site .. ..
 
BJ timu yetu ina matatizo makubwa sana. Haiwezekani upoteze wachezaji wazuri katika misimu mitatu/minne iliyopita VP, Adebayo, Fabregas, Kolo Toure, Gael Clichy and Samir Nasri, Song na kisha wale wapya wanakuja na viwango vya chini zaidi kuliko wale walioondoka. Management yote inabidi ifukuzwe ili kuleta mabadiliko ya kweli vinginevyo kuna hatari kama si msimu huu basi ujao timu ikashuka daraja. Inauma sana kuona timu ambayo ilihitaji wacheza wazuri watatu au wanne miaka michache iliyopita kuongeza nguvu na kujiweka katika nafasi nzuri ili kuweza kutwaa taji la EPL na UEFA sasa hivi inaporomoka katika kasi ya kutisha. Chezea ubahili weye!...


BAK sio swala la ubahili wala nini, mpira wa jana vijana walikuwa hawako 90 - 100% ndio Premier League hiyo huwezi kumwaga pesa kama Man City, au Chelsick or Man Utd na ukafikiri basi hiyo ndio neema. Judas alikaa miaka nane na ame perform mwaka moja .. .. .. let them go tunahitaji wachezaji wanaopenda kuichezea Arsenal na hakuna mchezaji ambaye ni bigger than the club. Rangers wako wapi? Chelsick wamefungwa jana, last few weeks Manure walipigwa ndio EPL hiyo lazima uwe 90 -100% kila mechi Ooops baki Manure ambao wanatumia bahasha etc. wanabebwa na mbeleko kama katoto kadogo .. .. usiwe na shaka msimu bado mrefu sana tutaona hii December itaishaje na huwezi kutoa judgement hadi May uone timu itakuwa wapi?

Wacha wanoko waseme lakini wanafahamu mziku wa prof ni mnene na hawawezi kuucheza ... ...

 
Back
Top Bottom