Arsenal wakamilisha usajili wa mshambuliaji Lukas Podolski.
Club ya Arsenal imekamilisha usajili wa mchezaji mshambuliaji wa kimataifa wa Ujerumani Lucas Podolski, ambao umegharimu kiasi cha £11 milioni. Mchezaji huyo bado yupo Ujerumani lakini pindi msimu wa ligi utakapoisha atakuwa mjini London kukamilisha taratibu zote.
Mkataba kamili unasemwa kuwa ni paundi milioni 5 kwa mwaka ambazo ni sawa na paundo 80,000 kwa wiki.
Lucas Podolski akiwa kazini.
Baada ya hapo kama nilivyowahi kusema huko nyuma Arsene Wenger ambae amesema wazi kwamba safari hii hatachelewa kufanya usajili, ataelekeza macho yake kwa Yann M'Vila mchezaji kiungo wa Rennes ya Ufaransa ambae atagharimu kiasi cha £15 milioni.
Yann M'Vila (kulia) akiwa kazini.
M'Vila ambae ana miaka 21 atakuwa asset kubwa kwa kumsaidia Alex Song ambae kuna wakati huonekana kuchoka na kuhitaji msaada ambao haupo kwenye eno la kiungo unganishi au "holding midfield" kazi ambayo imewashinda Abu Diaby na Francis Cquelin ambao bado hawajawa na uzoefu wa kutosha.
Arsene Wenger pia amepanga kuwaondoa wachezaji wote wasio na tija wakati wa summer kama Chamakh ambae anatakiwa na Juventus, Andrey Asharvin ambae timu alioko kwa sasa ya
Zenit St Petersburg inataka kufanya usajili wake uwe wa kudumu.
Pia Carlos Vela usajili wake na Real Sociadad utafanywa kuwa wa kudumu ingawa ameonekana kufanya vizuri kwenye ligi ya La Liga pamoja na ule wa Denilson Pereira Neves kule Sao Paulo Brazil na Nicklas Bendtner ambae yupo Sundeland.
Wachezaji wengine ambao ni kama hawapo na hata wakicheza huweza kuleta majanga na wapo kwenye sell list ni pamoja na Sebastian Squillaci, Johan Djourou Lucas Fabianski na Manuel Almunia.