Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,845
- Thread starter
- #81
Mnanikumbusha ile hadithi ya mchina alikuwa haelewani na mama mkwe wake, akaenda kwa mganga akiomba dawa ya kumwua. Mganga akamwambia nitakupa dawa inayoua taratibu kwa sababu kama akifa ghafla utashtukiwa. Mganga akampa majani yaliyosagwa vizuri akamwambia nenda mpikie chakula kizuuuuuri umwekee na hii daya kidogo. So kila siku ufanye hivyo na wewe umwonyeshe upendo yaani uwe naye karibu na umpe kila akitakaco. Akikutukana wewe cheka ni sehemu ya dawa so hata akijakufa watu hawatakushtukia wewe sana sana watakuonea huruma.
Bi dada akaanza kazi ya "kuua" akawa anajipikilisha vinono, anamcare yaani kuliko hata anavyomcare mumewe au mamake mzazi. Baada ya mwezi wakawa marafiki wa kufa yaani wakawa wanapiga story kupita maelezo. Ikabidi bi dada arudi kwa mganga amwambie anaomba dawa ya kupunguza makali ya sumu alokuwa anampa mama mkwe kwa kuwa kwa sasa hataki tena kumpoteza amekuwa rafiki yake mkubwa. Mganga akamwambia wala ile haikuwa sumu ni vitamins tu na kilichobadilisha tabia yake ni atitude yako na upendo na kujali unakompatia so endelea tu kuishi kwa furaha na rafiki yako.
So sometimes na sie wanawake tunapaswa kuangalia attitudes zetu towards wamama hawa. Ingawa nakiri wapo wale ambao hawapendeki yaani hata ufanye nini umlambe miguu kila asubuhi kama ishara ya kumshukuru kwa kukuzalia chema wapi.......atakubetulia mdomo. Mie huwa naangalia sana movie za kinigeria hasa zile za Patience Ozokwor "Mama Gee". akiamua kucheza kama mama mkwe mwenye roho mbaya huwa ananimaliza kabisa. But najifunza mengi
...MwanajamiiOne hili somo nimelipenda sana, busara tupu mydear, thanks. Hawakukosea waliosema " 'adui yako' mpende" au " 'mchawi' mpe mwana amlee!"
kaka Mbu umeniuliza chanzo cha mvutano, ni vijimambo vingi sana katika kutaka kuingilia mambo yangu ya ndani, na iliponitibua zaidi ni wakati nilipokofofishana na mr kwa kutaka niache kazi, baada ya kukosana amani ndani kwa karibia miezi 6 nikaja ambiwa chanzo ni mama yake kumshikia bango mr kwamba natakiwa niwe mama wa nyumbani, hilo tuliliongea na mr na tukasuluhisha kila kitu, baada ya hapo sasa mama akaanza kwamba cmtii mume wangu coz akitoa maamuzi ndani siyafatilii, hapo tulishaongea na mr kila kitu kuhusu mama, na akanipa support kubwa sana baada ya ule utata uliotokea, bac kwasasa support yake ndio inanipa moyo.
...Nyamayao, shukran kwa ufafanuzi murua na hitimisho zuri sana.
Nami nimejikumbusha hekima na busara aifanyayo mumeo hapo, hiyo support anayokupa.
Hata kama Mume mtu 'atauma akipuliza', so long as mama mzazi na mke watajiona wanapewa support, migogoro ya aina hii itapungua tu.
Huenda zile simulizi za busara; "kati ya baba, mama, mke na mwana nimuokoe nani?" pia zililenga kutatua migogoro kama hii :thumb: