MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,562
MJ1 naona unaongelea ndoa yangu, shemeji yako alikudokeza kitu?...mhh mama mkwe wangu habebeki jamani, hayo ya kutoka out na kila m2 anarudi kivyake ndio tunayoyafanya na mr mama akiwepo huku, jamani mama mkwe wangu cjui nimbebe na mbeleko gani, lakini cku hizi najitahidi kumwacha alivyo japo bila support ya mr nicngeweza, kwa mama mwanae ni kama bado anatambaa vile, hakuna mtu anaeweza kumwonyesha njia ya maisha zaidi yake yeye....
Hahahaha Mamiie wala usihofu hayako kwako tu haya lol umenichekesha lakini.
Una afadhali nyamayao kuwa Prezidaa wako anamuelewa mama yake wengine hawataki kuelewa na badala yake wanaside nao basi we mwana wa kuja unanyanyaswa hadi unashika adabu mwishowe unaona upuuzi unauvua utu wewe na kuanza malumbano, nyumba waigeuza uwanja wa mashambulizi ya wake wenza.
Bora mwakaa mbali mbali mwee!!....................
Mi nakwambia bibi yangu naye alikuwaga na yake, basi akikutana na mwanae wa kike (aliyetoka kwa mumewe kisa mama mkwe) wanamsimanga mama yangu yaani nilikuwa naumia ila vikizidi (hapo nlikuwa darasa la nne at) nawapaka.. na kuwazomea kitoto hayooooo hayana kazi kazi kumsema mama yangu .... na wao walivyokuwa na akili zao wenyewe wanatoka wananikimbiza ah..Siku hizi ni best kweli na yule shangazi lol.