Why Black Americans wapo hivyo? Sababu ya systematic Racism, haitokei tu ghafla watu wanabadilika bali ni mifumo ambayo imewekwa mamia ya miaka kuwakandamiza, wewe unaangalia juu juu then una Conclude ni watata.
Nitakupa Mfano wa Seedorf, hakuna mpenzi wa mpira kindakindaki asiemjua, midfield wa ukweli ambaye ameshinda Uefa za kutosha na timu tofauti tofauti,
Huyu jamaa baadae Akawa Kocha wa Ac milan kwenye kipindi kigumu, hakufanya vizuri wala vibaya average alikuwa na 1.59 points per match, toka Aondoke Milan mpaka leo Seedorf hana timu, mwenyewe akihojiwa vyombo vya habari anakwambia hata offer hapati.
At same Time kipindi hicho hicho Pipo inzaghi akawa kocha wa Milan sawa na Seedorf ila yeye alifanya vibaya zaidi, average point per match yake ni 1.38 japo Inzaghi alifanya Vibaya ameshapata kazi 5 timu tofauti tofauti ikiwemo Bologna, Reginna na Venezia, na kuna timu kibao kaharibu na bado anapata kazi, ila Seedorf kama hawamuoni japo Seedorf kama Mchezaji na Kocha ana Cv nzuri zaidi.
Sio tu Seedorf kina Viera pia wanaliongelea sana Sehemu zote zinazohusu decision making kwenye mpira nadra kukuta watu weusi, Viera anachofanya Palace pale ni kikubwa sana i doubt kama kuna timu kubwa inamtaka, ukienda kwenye Ma CEO, na Executive wengine wa juu wa mpira ngumu kwa mtu mweusi kutoboa.
So kama system ipo programmed hivi kwanini Doctor, Engineer na wengineo wanaokosa nafasi wasijisikie kutengwa na kuwa watata?